Washiriki wa Redd's Miss Higher Learning Dodoma 2012, wakiwa katika picha ya pamoja katika kambi yao ya mazoezi iliyopo katika Ukumbi wa NK Club mjini Dodoma leo. Warembo hawa watapanda jukwaani Ijumaa hii kuwania taji hilo.
Warembo 11 wa Redd's Miss Higher Learning Dodoma wanataraji kupanda Jukwaani May 18,2012 katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma kuwania taji hilo kwa mwaka huu.
Show hiyo inataraji kuzindikizwa na Mwimbaji bora wa Kiume wa Tuzo za Kili Music Award 2012, Barnaba kutoka kundi la THT ambaye kwa sasa anawika na wimbo wake wa Magubegube.
Shindano hilo mbali na kudhaminiwa na REDD'S, pia limepata udhamini wa Nokia, Star Time, Nina’s Fashion, Shabby Bus, Clouds FM, African Dream, Club 84, Radio Kifimbo, Salama Salon, Jambo Leo, Mapouder Cosmetics, Emage For You, Salome Boutiq, Dicentman Blog, Joseph Lukaza Blog, na CafĂ© La’Tino.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...