Wadau wakijikoki kabla ya kuanza matembezi hayo ya hisani

Watanzani wakipeperusha bendera ya Tanzania katika Matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na jiji la Yokohama
Mwenyekiti wa watanzania wanaoishi nchini Japani Radhid Njenga (mwenye kanzu) naye alikuwemo.

Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, wamewaongoza watanzania wanaoishi hapa kushiriki katika matembezi ya hisani ya mji wa Yokohama, ikiwa ni moja ya hatua za kukuza urafiki kati ya jiji hilo na Tanzania.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na hata mataifa ya Afrika kushiriki rasmi kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka. Mwaka huu, Tanzania kutokana na historia yake ya kupenda, kusimamia na kutetea amani, umoja na mshikamano duniani.

Aidha katika siku za usoni, mji wa Yokohama una mpango wa kuanzisha uhusiano (Sistercity Friendship) na moja ya miji ya Tanzania, uhusiano ambao utajumuisha kupanda miti aina ya Cherry blossom katika mji utakaochaguliwa Tanzania.

Matembezi hayo yalianzishwa mwaka 1953 kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kufufua uchumi na utalii wa mji wa Yokohama kufuatia uharibifu uliotokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2012

    Safi sana lakini kwani hakunaga mavazi mengine ya Ktz? Mbona mnaiga haya ya kwetu wamasai? Wachaga wangedumisha mila yao, wahaya, wasukuma, wanyamwezi, wafiome na wakerewe. Kila mahali watz wakienda now is Masai calture utafikiri ndo vazi la taifa, Angalieni wanaigeria wanapendaza na mavazi yao ya kujichanganya. Tuachieni mavazi yetu ya kimasai maana hata kufunga hamjui

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...