Waziri wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi kitabu cha sheria na mwongozo wa utendaji kazi wa wizara hiyo Waziri Mpya Dkt. Hussein Mwinyi.Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Waziri Dkt. Mwinyi akipokea kitabu cha utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo ambapo ameahidi kuendeleza kutekeleza na kuendeleza majukumu yale aliyoyaacha ingawa anatambua changamoto kubwa ni kuboresha huduma ya afya upande wa tiba.
Mawaziri hao wakipeana mkono mara baada ya makabidhiano hayo Dkt. Mponda amemtaka waziri Dkt. Mwinyi kufuatilia na kusimamia vyema utekelezaji wa mikakati ya sekta ya afya ili kuweza kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi aliyekaa katikati,Kulia ni waziri wa zamani Dkt. Hadji Mponda na Naibu Waziri Mpya Dkt. Seif Rashid aliyekaa kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hiyo mara baada ya makabidhiano ya ofisi.(Picha na Catherine Sungura-Mohsw)
Pole Dr. Hadji Mponda.
ReplyDeleteInasikitisha sana lakini ndio ilivyo yameshakuwa!
Anaonekana ni mtu mstaarabu sana, haya inabidi uyakubali mabadiliko na majaribu na sasa unarudi Darasani(Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili-MUHAS) kwenda kufundisha!
-Unaweza kuwa na Mali ukafilisika,
-Unaweza kumiliki kitu kikakutoka,
-Unaweza kuwa na Madaraka yakatoweka,
-Unaweza kuwa na mwana akaenda mbele za Haki!
MWISHOWE UKABAKI UNALIA NA NAFSI!
WAZARAMO WALISEMA 'MULUNGU CHIBIDU!'
Pole Dr. Hadji Mponda!
ReplyDeleteWala usijali Mungu atakupa kingine.
Daktari Hadji Mponda,
ReplyDeleteUnalo Genge?,
Unamiliki mabasi ya Daladala,Teksi au Boda boda?
Una mbuzi,kuku,bata na ng'ombe? au Shamba?
Kama huna ni bora upande ndege wende zako Majuu ukafundishe Vyuo Vikuu huko!
Jamani tuwaonee huruma Mawaziri Waliotolewa !
ReplyDeleteHakuna kitu kinaumiza na kutia simanzi kama moja ya haya hapa matatu (5):
1.Kufilisika kwa mali
2.Kufiwa na mtu kipenzi wa karibu
3.Kuanguka madaraka
4.Kusalitiwa ktk Mapenzi
5.KUBWA LAO (Kuthibitika iwe kwa matokeo ya Vipimo au kutambua ya kuwa sasa umeathirika kwa Ukimwi au Kansa)!
YOTE TISA YANAUMA ILA MAUMIVU MAKALI ZAIDI YA NO.(5) NA NO.4 HAPO JUU (KUATHIRIKA,KUSALITIWA MAPENZI) INAUMA ZAIDI NI NAMBA TATU (3)...YAANI KUANGUKA KIHESHIMA NA MADARAKA!
Dr.Hadji Mponda anajikaza kisabuni ila anatia huruma sana!
Madaraka na Mapenzi yana RAHA na KARAHA!
ReplyDelete1.MADARAKA:
Kuchaguliwa kupata Madaraka KUTAMU KAMA ASALI!
Kulega lega kwa Madaraka KUCHACHU KAMA LIMAO!(Kipindi cha migogoro ya Madakitari)
Kuondolewa kutoka Madarakani KUCHUNGU KAMA SHUBIRI!
2.MAPENZI:
Kumpata mpenzi mpya au ndoa Changa KUTAMU KAMA ASALI!
Kulega lega kwa Mapenzi au Ndoa KUCHACHU KAMA LIMAO!
Kuvunjika kwa Penzi ama Ndoa KUCHUNGU KAMA SHUBIRI!
EWE MOLA KWA MASAHIBU HAYO MAWILI HAPO JUU NO.1 NA NO.2 UTUPE SUBIRA!!!
Hivi hakuna njia ya Busara zaidi ya kuwatoa watu ktk kazi zaidi ya kuumbuana kama hivi?
ReplyDeleteInakuwa kama ndio basi tena na kuwa labda mtu huyo hana umuhimu kabisaaa, kitu ambacho sio kweli!
Napendekeza wanaotolewa kazini waitwe kwanza kabla ya zoezi zifanyike hatua hizi:
1-Waelezwe makosa yao,
2-Wajiuzulu,
3-Wakabidhi Ofisi (Kwa faragha/ siri) kwa Watumishi wapya,
4-Halafu wasafirishwe nje ya nchi
5-Na huku nyuma ndio itangazwe!