Ubao ulivyokuwa unasomeka baada ya Yanga kupigwa na Simba mabao 5 kwa nunge katika Ligi Kuu ya Vodacom, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jioni ya leo.
Wachezaji wa Simba wakishagilia ubingwa baada ya kukabidhiwa kombe na Waziri Mteule wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala |
Waziri Mteule wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala (kushoto), akimkabidhi kombe la ubingwa wa Tanzania Bara baada ya mechi na Yanga kumalizika leo kwenye Uwanja wa Tgaifa, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)
Wachezaji wakifurahia kombe |
Simba wakishangilia ubingwa kiaina
Kocha wa Simba Milovan Circovic akiwa amebebwa na wachezaji |
Wachezaji na viongozi wa Simba wakicheza mduara baada ya kuifunga Yanga mabao matano na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara |
Wapenzi wa Simba wakishangilia ushindi wa mabao matano dhidi ya Yanga pamoja na ubingwa
Ni furaha kwa Simba kila mahala.
Picha na Kamanda Richard Mwaikenda
Mkono mmoja wenye vidole vinne watosha kuisambaratisha yanga na kuzidisha kizaazaa jangwani.
ReplyDeleteAminia Simba Taifa Kumbwa.
safi sana simba hongereni mnooo
ReplyDeleteKazi ya ukocha ni taaluma. Hivi miziro taaluma hii kaipatia wapi? Yanga ubishi kubishana na wenye taaluma zao. Matokeo yake ni kutunguliwa 5-0.
ReplyDeleteTulisema kaa mbali na Simba.Hii ndo Simba ya Afrika na subirini makubwa zaidi.
ReplyDeleteHongera Simba,hongera viongozi,na hongera wanachama na wapenzi wote wa Smba.Umoja wenu umelipa.
Yanga hawakuwepo uwanjani nini?
ReplyDeleteHii ndio tofauti ya soka la kitabuni na soka la gazetini.
ReplyDeleteKabla ya mechi walisema sana ubingwa wameukosa lakini wataingia uwanjani na kulinda heshima yao. Na kweli! Umma umejua kiwango cha heshima yao kilipo.
Hongera sana wekundu wa Msimbazi. Sherehekeeni leo lakini msibweteke. Mechi nzito za Afrika zinakuja.
Dah!! yaani hapa raha tupu...ubingwa na kumpiga Yanga bao 5-0...natamani ningekuwepo hapo uwanjani
ReplyDeleteMdau US.
Michuzi mbona nasikia mechi ilichezewa mezani ili kumkomoa Mwenyekiti baada baadhi ya wafadhili kumtaka aondoke na yeye kukataa. Kwa walioangalia mechi uvumi huu waweza kuwa kweli
ReplyDeleteIvi mwanume anapopigana na mwanamke akampiga hujisifia kweli?!! Ivi na nyie kwa akili zenu mnaona Yanga kuna timu ya kushindana na Simba akujipima kiwango kwa Simba mpaka Simba wakashangilia ushindi kwa kishindo!
ReplyDeleteSimba ingepambana na wanume ndo itambe we unapambana na Yanga watoto wa kike unajitapa kama mjinga!
Yanga ilikuwa zamani lakini sasa hakuna Yanga labda wajipange upya na vitu vipya na uongozi mpya.
duh huwezi amini yanga leo imetunguliwa 5-0 vichekesho ujue nn imedhihirisha ni kiasi gani kiwango chao kimekuwa. hongera sana simba mko juu kip it up
ReplyDeleteHizi bao 5-0 amefungwa Mjomba Muhidin Issa Michuzi kada wa Chama cha Mapinduzi, pamoja na Mchezaji NAMBA 1 wa Yanga Mhe. JK !
ReplyDeleteDuhh gharika imetua Jangwani-2012 !
ReplyDeletePoleni Mhe. JK na Mjomba Michuzi kwa kipigo cha 5-0 !
Kibelaaaah
ReplyDeleteKuna mdau mmoja juzi wakati azamu alipopigwa na Mtibwa akasema simaba wamepata ubingwa wa mezani a.k.a wa kusubiria matokeo ya wengine na alihitimisha hivi:
ReplyDeleteni kama majizi yamekurupushwa sehemu fulani halafu wakati yanafukuzwa yakaukuta mlago wako uko wazi wakati huo ww unaota kupata mipesa kisha unaamka unakuta hiyo mijizi iliyokurupushwa mahali imekuachia kapu la pesa.Sasa nataka kumsikia tena huyo mdau atuambie hiyo MIJIZI ilikuwa ni YANGA a.k.a kandambili!??