Bi Helena Mteti Meneja Muhakiki wa Kodi Airtel akipata ushauri kutoka kwa muugizi Bi Elizabeth Mgaya kutoka kitengo cha damu salama cha taifa kabla ya kuanza zoezi la kuchangi damu lililoandaliwa na Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel likishirikisha wafanyakazi wake. Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika siku nzima leo katika makao makuu jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Airtel Bwana Greyson Mapunda akijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa Airtel kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu. Zoezi hilo la kuchangia damu lilifanyika jana siku nzima katika makao makuu Moroco. akitoa huduma ni Bwana James Semba kutoka Kitengo cha damu salama cha taifa
Wafanyakazi wa Airtel wakijitolea damu katika zoezi la kuchangia damu lililoandaliwa na kuhusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kuchangia damu kwa mfuko wa taifa wa kuhifadhi damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...