There is no more lovely, friendly and charming relationship, 
communion or company than a good marriage".

KUMI NA TANO SI HABA (PONGEZI)
Pongezi nina zituma, kwako Tedi nawe Nesto
Mu imara kama chuma, kwa upendo wake Kristo
Mungu awape uzima, mkalea na watoto,
Kumi na tano si haba, Mroki nawapongeza.

Mroki nawapongeza, kumi na tano si haba, 
Nesto leo umeweza, nyumbani waitwa baba,
Tedi  ye hakuteleza, tuli yeye hakuyumba,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Mungu kawabariki, wana weri kawapa,
Japo home hamshikiki, ulinzi wana huwapa,
Ibada mnashiriki, pongezi mi ninawapa,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Kubwa shukrani kwa mola, mja wetu wa karima,
Alo ziepusha hila, kwetu sisi maamuma,
Tedi waivaa shela, hakupenda dada wema,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Jala wetu wa Jalalu, wape zaidi hekima,
Mmoja asiwe lulu, mwingini akawa Kima,
Hapo hawatafaulu, kuheshimiana daima,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Wote mkajidhatiti, kwenye wenu upendo,
Mkipiga Serengeti, msipigane mabindo,
Kuweni watu wa geti, upole uwe mtindo,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Hizi saba zinatosha, kiu kimenikamata,
Sio vyema kuwachosha, maneno mmeyapata,
Nami nitajibidisha, yenu siri kuipata,
Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

Mroki Mroki “Father Kidevu
+255 717 002303
mrokim@gmail.com
www.mrokim.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2012

    Siwajuhi wana ndoa; ila nawapa pongezi pia. Miaka kumi na tano si mchezo; kuna kina Monica Reille Lewinsky na kina Hunter wengi tu kwa sasa Tz. Mumtangulize Mungu; hakika kifo ndicho kitakachowatenga.

    ReplyDelete
  2. Nami zangu pokeeni, za upendo na hongera,
    Muwe hadi uzeeni, mmesimama imara,
    Hadi leo si utani, ndoa yenu inang'ara,
    KUMI NA TANO HONGERA, MUWE NYOTE MAISHANI.

    Waombea kwa WADUDI, kila jema maishani,
    Nesto umlinde Tedi, chochote sije mkhini,
    Upendo wako uzidi, akhisi yupo peponi,
    KUMI NA TANO HONGERA, MUWE NYOTE MAISHANI.

    Nesto wakadhalika, nasema toka moyoni,
    Lolote sije udhika, umsamehe mwandani,
    Si haba mlipofika, YARABI akulindeni,
    KUMI NA TANO HONGERA, MUWE NYOTE MAISHANI.

    Waombea kila jema, ya kheri yawe usoni,
    Na wana mlee vyema, kama RABI kakupeni,
    Wenye shari wanadama, MOLA kunusurisheni,
    KUMI NA TANO HONGERA, MUWE NYOTE MAISHANI.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2012

    kwani blog yako haisomwi ndio unaweka huku.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2012

    5th anniversary: Wood/Associated Flowers: Daisies
    In Wales, elaborately carved wooden 'lovespoons' have been given for centuries. The term 'spooning' - meaning 'romancing' - originates from this Welsh tradition. An alternative gift to each other could be a romantic vsit to a log cabin

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2012

    mmmh, mie napita tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2012

    MIE NIMETIMIZA 15 JUZI JUZI TU. HONGERENI NA NYIE

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2012

    Congratulations

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...