Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Kwa hili lazima tulikemee la kuvunja sheria za nchi na halmashauri kwa baadhi ya wanasiasa kuwaambia watu kutolipa fedha za taka na kutohama sehemu za kingo za barabara na mabarazani mwa maduka sanjari na nje ya masoko yetu wanakofanyabiashara jijini Arusha.
 Kumekuwa na wimbi kubwa la uvunjaji wa sheria na kila halmashauri ikiwataka kuhamia kwenye masoko yaliyojengwa kwa nguvu zetu sisi wenyewe hukataa kwa madai kuwa kuna mwanasiasa amewaambia waonyeshwe kwanza pakwenda wakati teyari halmashauri imeshawambia mahali pa kwenda huku ni kuvunja sheria tulizojiwekea.
 Jiji la Arusha lenye sifa ya kuwa jiji la utalii limekuwa dampo sasa kwa kila anayetaka kufanyabiashara kufanya biashara sehemu yeyote mradi apate maslahi yake.
 Ukipita soko kuu la jiji hili utajionea biashara zinafanya hadi kwenye kingo za barabara na kila halmashauri inapotaka kuwaondoa wamekuwa wanapigana na mgambo na wengine kubeba mapanga huku ndiko tulikofikishwa na wanasiasa wa majitaka.
Tufike mahali tukemee kwa nguvu zetu hali hii kwani inataka kulifanya jiji letu kuondokana na sifa ya kuwa jiji la mfano hapa Afrika ya mashariki kwa kuliundia sheria ndogo ndogo ambazo teyari mwanasheria wetu wa halmashauri ameziainisha kwa ajili ya mchakato wa maoni yanayoendelea kutolewa.
 Wananchi wasiwe wakwanza kuvunja sheria na kuwaogopesha viongozi kusimamia sheria za nchi kwa kutaka maslahi yao ilimradi wamevunja sheria nasi tukabaki kuwaangalia bila ya kutimiza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria za halmashauri.
 Kumekuwa na ujenzi holela unaofumbiwa macho na wakuu wa idara za halmashauri yetu kiasi kuwa jiji hili limekuwa na ujenzi wa makazi ya watu kwa kasi ya ajabu kuliko majiji yote hapa nchini bila kufuata mipango miji nasi kuendelea kukaa kimya na sheria zinavunjwa na wachache kwa maslahi yao binafsi.
 Wimbi la upandishaji tozo ya majengo kiholela nayo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa ni kitanzi kwa wananchi na kuwatakiwa mwanasheria kubuni  njia mbadala ya kuwafanya watu kulipa tozo hizo za sasa kabla hawajapandisha tozo nyingine kwani wameshindwa kuonyesha hata data base ya halmashauri hii nayo ni uvunjaji wa sheria zetu tulizojiwekea.
 Ukusanyaji wa tozo hapa ni tatizo siyo kuongeza tozo tufike mahali tuangalie makusanyo yetu yanakidhi vigezo tulivyojiwekea au la ndipo mwanasheria atuambie suala zima la kuongeza kodi ya majengo.
 Wananchi na viongozi wetu tukae na kujadili wapi tunapoelekea badala ya kutafutana uchawi huku tunaendelea kuvunja sheria na kuundiana sheria kwa kukomoana bila ya kuangalia vipato vya wananchi na kushindwa kukusanya mapato ya halmashauri isiwe ndiyo kigezo tukusanye kwanza tuone halafu kama kuna upungufu ndipo tuweze kuongeza tozo.
 Wakazi wa jiji hili hasa wafanyabiashara tuwe macho na kuacha kuvunja sheria za nchi kwa kukataa kutii sheria za kuhama kwenda kwenye masoko mapya je hatujali fedha zetu tunazo tozwa na halmashauri tusiwe wa kwanza kuvunja sheria za nchi kwa maslahi binafsi ya wanasiasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2012

    Chadema Arusha kazi kwenu!

    Si mlilia chai sasa ndio ninyi tena mnalalamika mnaungua?

    Ni aina gani ya Uendeshaji wa Ustawi mnaoufanya enyi Serikali ya Kisiasa ya Arusha iliyo chini ya Chadema?

    Arusha ndiyo mnavyoiendesha Kiswahili namna hii?

    Mkumbuke Arusha ndio Makao ya Shirikisho la Afrika ya Mashariki!

    Kama ingekuwa ni kazi ya CCM mngesema nini utaratibu mbovu wa uendeshaji wa Mji muhimu nchini kama Arusha?

    Arggghhh!!!!,

    Acheni Siasa za ubabaishaji!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    Hali ya Arusha ni ya kukatisha tamaa. Siku hizi siendi kabisa soko la kilombero. Bidhaa zimepangwa hadi njiani, takataka, wabeba rumbesa wanapishana, ni vurugu na hatari kwa afya ya muuzaji na mnunuzi. Vibaka pia wanakazi uzi. Kuvuka barabara pale kilombero ni kazi. Hili liangaliwe.
    Mimi nimesoma shule ya Ngarenaro primary enzi zile soko la kilombero lilikuwa safi bidhaa fulani ziko ndani ya soko na zingine nje ila zinapangwa juu ya meza. Kulikuwaga kuna mto kira kira unaotenganisha soko na shule. Kulikuwa na eneo la green pembeni mwa mto. Siku hizi mto umekauka biashara mpaka kwenye bonde la ulipokuwa mto. Uchafu kila mahali. Hii ni aibu kwa jiji la Arusha. Enzi hizo ilikuwa inawezekana kutembea kwa mguu kwenda mjini. Sasa hivi makelele, vifodi kila kona, vitoyo. Vurugu. I miss the old Arusha, small, green clean and friendly.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2012

    Kinachoniudhi sana Arusha ni (1) machokoraa - watoto wa mitaani wanaovuta bangi na kunusa gundi mbele ya mapolisi city centre,
    (2) wauza batik wanaowasumbua watalii na/au wazungu ambao hawataki kununua vitu vyao na (3) flycatchers ambao ni 'mawakala' wa makampuni ya kitalii ambao wanawasumbua wageni. Mzungu hata akisema hataki kwenda Ngorongoro au kununua batik atagandwa mpaka achoke!Mamlaka husika lazima zichukue hatua muafaka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2012

    CHADEMA comments zote 3 hapo juu zinawachana ninyi!

    Arusha inawashinda, leo tena mnadai kupewa nchi nzima si mtairudisha Tanzania enzi za Ujima katika karne ya 12 wakati tunaelekea karne ya 21 ???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2012

    Mbona this sounds like Dar? na li Dar nalo liko hivihivi!!!! kila mtu anafanya biashara popote anapotaka!!! hakuna cha site wala nini! na Dar wala sio chadema!!!

    Hili sio suala la chadema wala kitu gani sijui, hata sijui ni kitu gani! Maana hii kero ya kuchafua miji eti watu ''wapate mikate yao'' IMEZAGAA NCHI NZIMA!!!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2012

    Umachinga mpaka Arusha Uswisi ya Afrika?

    Hii hapana,,,haya mambo ya kutitumia Siasa ili kula yanatakiwa yafikie mwisho tukianzia miji yote mikubwa Mwanza,Mbeya, Dar Es Salaam na hii 'uzunguni' yetu inayotuingizia Dola $$$ lukuki, ambayo ni Arusha!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2012

    Angalieni ahadi za Uchaguzi 2010 katika Siasa za Kiusanii!

    Hivi Arusha Wapiga kura hizi ndizo 'ajira' mlizo ahidiwa Oktoba 2010 wakati wa Uchaguzi?,,,(Umachinga wa kutandika magunia chini kwa kuuza bamia na vitunguu)

    Ohhh bora mngebaki na CCM labda mipango ya Madini ya Tanzanite mngerejeshewa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...