Mshambuliaji wa timu ya mkoa wa Kilimanjaro, Adam Soba akiwatoka mabeki wa Shinyanga katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume wa mashindano ya Copa Coca-Cola. Kilimanjaro imeshinda 2-0.
Ilala imeendelea  kufanya vibaya kwenye michuano ya Copa Coca-Cola baada ya leo asubuhi  (Juni 28 mwaka huu) kuchapwa mabao 4-0 na mabingwa watetezi Kigoma  katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar  es Salaam.
Mabao yote katika  mechi hiyo ya kundi A yalifungwa kipindi cha kwanza huku Ramadhan Salum  akipiga hat trick (mabao matatu). Alifunga mabao hayo dakika ya 13, 43  na 45. Bao la pili kwa washindi lilifungwa dakika ya 19 na Athuman  Rashid.
Wakati Kigoma  imeshinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza mpaka sasa katika kundi  hilo, Ilala imepoteza mechi zote tatu ilizocheza. Ilala imefungwa na  Arusha, Kigoma na Lindi wakati mechi yake inayofuata itakuwa Juni 30  mwaka huu dhidi ya Kusini Pemba.
Nayo Kilimanjaro  imeendelea kufanya vizuri katika kundi lake la D baada ya leo asubuhi  (Juni 28 mwaka huu) kuitandika Shinyanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa  Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Mabao ya  Kilimanjaro ambayo hadi sasa imeshinda mechi mbili na kutoka sare moja  yalifungwa na Adam Soba dakika ya 11 na 46 wakati la tatu lilifungwa  dakika ya 81 na James Henry. 
Katika mechi  nyingine zilizochezwa leo asubuhi (Juni 28 mwaka huu), Temeke na Mtwara  zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Ali  Makalani alianza kuifungia Temeke na baadaye Adam swaleh akaisawazishia  Mtwara. 
Uwanja wa Nyumbu  mkoani Pwani ulishuhudia Morogoro na Kaskazini Pemba zikitoka sare ya  bao 1-0. Amin Kassim aliifungia Kaskazini Pemba dakika ya 51, na  Morogoro wakasawazisha dakika ya 75 kupitia kwa Mutalemwa Katunzi katika  mechi hiyo ya kundi B.
Mechi  zitakazochezwa leo jioni (Juni 28 mwaka huu) ni Lindi vs Arusha  (Tanganyika Packers), Manyara vs Mjini Magharibi (Nyumbu), Kinondoni vs  Mbeya (Tamco) na Kusini Unguja vs Pwani (Karume).
Kesho (Juni 29  mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea tena Juni 30 mwaka  huu kwenye viwanja vyote vinne.
VODACOM  KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI JUNI 30
Kampuni ya Vodacom  itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012  katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double  Tree Hilton jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo  itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu  itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo  bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu.
Wengine  watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu,  mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora. 

Boniface Wambura
Ofisa  Habari
Shirikisho  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...