Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi yake Said Shaabani mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.kutoka Ziara ya wiki Tatu za nchi za Israil,Cuba na UAE.
Makamu wa PIli wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali IDI akisalimiana na Mtoto wake Mdogo mara baada ya Kuwasili kutoka katika ziara ya Nchi za Izrail,Cuba na UAE.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akijibu hoja mbalimbali za waandishi wa Habari waliofanya mahojiano nao mara baada ya Kuwasili kutoka katika ziara ya Nchi za Izrail,Cuba na UAE.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI ALI-HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
La haula, mimi nilifikiri nilichelewa kuanzisha familia,kumbe wala!
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.
Wewe Dr Bitozi utakuwa ulichelewa tu. Labda ungeuliza huyo ni mke wa ngapi? Wenzetu wanaoa wake wanne. Vilevile kwa utamaduni wao TARAKA ni njenje. Akifanya kosa la kwanza anapewa taraka ya kwanza, la pili taraka ya pili, la tatu Kwa heri ya kutokuonana. Na hapo inakuwa imepatikana 'space' ya kuoa mke mwingine
ReplyDeletewe anon wa pili TARAKA ndiyo nini? ni talaka, humo darasani yaelekea ulikuwa full kilaza maana umerudia hilo neno zaidi ya mara mbili, halafu uache uongo ati talaka nje nje, punguza pumba wewe.
ReplyDeletefrom canada
Wewe mzembe wa Canada vipi? Si umeerewa rakini? Au ukweri umekuuma? Mimi ni mkurya jamani. Natumia sana 'R' badara ya 'l'. Samahani kwa usumbufu huo. Rakini, ni kwa sababu ya eneo ninarotoka.
ReplyDeletekaka wacha masihara taraka sio kama ulivyosema eti taraka "ni njenje akifanya kosa la kwanza anapewa taraka ya kwanza, la pili taraka ya pili, la tatu Kwa heri ya kutokuonana"
ReplyDeleteKuna kusameheana na kuelimishana ii muishi kwa amani na upendo. kwani taraka ni katika mambo anayochukia muumba.
haha haha, nilidhani nimeshangaa mwenyewe huyo mtoto mdogo! au mwandishi kakosea?
ReplyDeletemkurya pore sana kwa rafudhi!
Huyo siyo mtoto wake huyo ni mjukuu wa mkewe Bi Asha. Msiwe mnaandika tu vitu hamvielewi.
ReplyDelete