Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifungua mafunzo maalum yaliyo andaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kuchambua Bajeti ya serikali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Mhe. John Cheyo na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovick Uttoh.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Uttoh akitoa neno la Utangulizi kabla ya kufunguliwa kwa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge kuchambua Bajeti ya serikali iliyo andaliwa na Ofisi yake na Kufanyika Bagamoyo leo.
Baadhi ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mhe. Spika wakati wa mafunzo maalum yaliyo andaliwa kwa ajili yao na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo kuchambua Bajeti ya serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.
Mgeni Rasmi, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti na makamu wenyeviti wa kamati za Bunge wanaohudhuria mafunzo maalum yaliyo andaliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwajengea uwezo kuchambua Bajeti ya serikali, yaliyofanyika Bagamoyo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2012

    Mi naona kama Mhe Makinda is overworking herself? Ziara, ugeni wa heshima kama zimezidi kidogo kwake. Kulikoni?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2012

    Mama Anne,pole na kazi.Umependeza sana, unaonekana kama binti wa miaka 28.Keep well Anne.Michuzi ukikaa mwenyewe kwenye comments unabana sana comments zangu nyingi,wakiwepo wasaidizi wako comments zangu zinaenda hewani...unabana sana zile za kuikosoa serikali.Mimi sijali sana mkuu,tutakutana Break point ya city centre kwenye ugali wa muhogo na nyama ya nyati he he he heeeeee..I know you mate

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...