Mla vichwa maarufu nchini Abdallah Bitebo (pichani) amesema kwamba yeye ni Hair Designer (mbunifu wa mitindo ya nywele) na sio kinyozi. Akiongea na Globu ya Jamii leo katika makao makuu ya kampuni yake iliyoko Magomeni Mapipa 'Lango la Jiji' jijini Dar es salaam, Bitebo kasema kinyozi ni yule anayekaa chini ya mwembe na kunyoa watu kwa kutumia wembe na mkasi, wakati yeye ni Hair Designer kwani sio tu hutumia vifaa vya kisasa katika kunyoa, bali pia ni mbunifu wa mitindo kama vile kupiga blaki, kuweka wave, kunyoa kwa kutumia mafuta maalumu, ku-scrub, kutengeneza kucha na kusugua magagana ya miguu na kadhalika.
Hata hivyo amewasifia sana vinyozi kwa kusema kuwa wanastahili pongezi kwa kuweza kufanya kazi kwa umakini, saa ingine kunyoa kwa kutumia kitana na wembe tu. "Vinyozi wengine ni shauri ingine kaka, maana wanakunyoa kwa mkasi na wembe na saa ingine kwa kitana na wembe tu nawe unatoka pale chini ya mwembe freshi kabisa.
"Ila sie hapa bwana ni ma- designer na sio vinyozi maana wembe na mkasi tunatumia kumalizia ubunifu wa mtindo ambao mteja anataka", kasema Bitebo, ambaye saluni yake ina wafanyakazi wapatao tisa, wakiwemo kinadada mahiri wa scrub, kuosha pamoja na manicure na pedicure. Pia ana tawi lingine la Bitebo Hair Designer jirani na kituo cha basi cha Mwananyamala KomaKoma.
Pia yeye ni mbunifu wa mitindo ya nywele pekee nchini anayepata tenda za kwenda kufanya kazi nchi za nje kwa mikataba mifupi - hasa wakati wa harusi hususan nchi za uarabuni na Ufaransa. Ni hivi majuzi tu alikuwa Abu Dhabi kwenye tenda ya kumnyoa bwana harusi na nduguze kibao. Pia mastaa wengi wa Bongo Movie na kandanda, ukiondoa viongozi kibao wa vyama na serikali, hunyoa kwake.
"Siri ya mafanikio yangu ni nidhamu ya hali ya juu, kastama kea babu kubwa pamoja na usafi wa sehemu ya kazi na vifaa kwani bila kuwa na vitu hivyo afadhali ufanye biashara ingine", alimalizia Bitebo, huku akiangalia foleni ya wateja waliokuwa wanaangalia Kombe la Ulaya huku wakinywa kahawa inayotolewa bure hapo.
Bitebo na wenzie wakiwa kazini
Kinadada wakihudumia wateja
Watu sita wanapata huduma kwa mara moja
Usafi na nidhamu
Kinadada wa kwa Bitebo wakiongozwa na Bi Mariam (wa pili kushoto)
kinyozi wa mitindo. lugha gongana hehe
ReplyDeleteHata hivyo kwa staili ya saa hivi naona bongo wameweka masister do wa kuosha na mbaya zaidi wako na cabin zao.cha kusikitisha ni kwamba asilimia kubwa ya masister do hao hawafanyi kazi zao.wakishaosha vichwa vya wanaume huwa wanafanya kujivuta kusisimua wanaume bila kujali kama wanaowahudumia wengine wana wake zao,kuna wacha mungu na wanaojiheshimu kwa ujumla.wapewe elimu ya ukimwi na maadili ya kazi kabla ya kufakamia kila wanaemuona.samahanini ila inakera .imenitokea mara kadhaa.
ReplyDeleteHata house girl unaweza kumuita home economics and nutrition specialist BITEBO ni kinyozi asikatae
ReplyDeleteKinyozi ni kinyozi tu, na yule wa chini ya mwembe bado anategemewa na asilimia kubwa ya watanzania.
ReplyDeleteDr Gangwe Bitozi.
HUYU BITEBO WA KUJA NINI?
ReplyDeleteAU KAJIFUNZA KIZUNGU UTU UZIMANI?
AU KISWAHILI PIA HAKIJUI?
NDIO HAWA HAWA BADALA YA KUVIITA "VITAFUNIO" WANAVIITA "VITAFUNWA"
BITEBO ACHANA NA USHAMBA NDUGU YANGU, WEWE BADO NI KINYOZI TU, HATA KAMA UNANYOA NYWELE ZA KWAPA.
Mdau Ukerewe
Kiswahili fasaha mtu naenyowa watu ni KINYOZI. Labda tuseme au tukubaliane, haya majina ya Hair Designe e.t.c. yanakuja kutokana na kwenda na wakati na mazingira tuliyo nayo sasa, zamani Kinyozi hata uchochoroni tu kazi yake inafanyika na analifurahia jina la kazi yake, siku hizi tu, kwa vile kuna hayo masalon ambapo baadhi yake unakuta pia mna 'beauticians' either wa manicure/pedicure na kuwa kama biashara, kadhalika majina kubadilika ya watenda kazi hiyo na sehem za kazi yao (Hair desighne na Salon). Ila ingekuwa miaka kadhaa ya huko nyuma, jina ni lile lile asilia KINYOZI. Hata hivyo kazi ni kazi, jina la kazi halimshushii mtu hadhi yake na wala halitilishi aibu. Ila huo usemi uliotumika hapo, ni sawa na mtu kusema ni Messenger siyo Tarishi.
ReplyDeleteMBALI YA MAJINA YALIYOTUMIKA CHA MSINGI NI KUWA HATA SISI TULIOPO HUKU UGHAIBUNI TUNAJIVUNA KUONA NCHI YETU INA VINYOZI (HAIR DESIGNERS)WENYE SALOON ZA LEVEL YA HALI YA JUU HATA HUKU KUNA NYINGINE HAZIIFIKII.HONGERA WABONGO NA KIDOGO KIDOGO TUTAFIKA CHA MUHIMU NI KUWA KILA TUKIONA KITU KIZURI KAMA HIKI TUWE TUNAKISIFIA ILI TUANZE KUUJENGA ULE MOYO WA KUPENDA VITU VYETU. TUWACHANE NA ULE UPUUZI WA KILA WAKATI KUTAFUTA KITU KIBAYA ILI TUANZE KUNANGA.
ReplyDeleteKazi nzuri niile inayokuingizia pesa kwa faida,na uzuri salon zina risk ndogo mno hivyo ukiitwa kinyozi fajirika bz nikazi isiyo babaisha bz ufundi na matokeo huwa nipapo kwa papo sio akinawenzangu kasha kula hela kisha mzigo hajakamilisha. Ukiona MTU anaogopa kuitwa kinyozi ujue hajitambui yani haipendi kazi yake na akijidanganya kuwa ni mwelevu mno au kasoma sana basi ni msomi asiejitambua ktk eneo hili. Big up vinyozi kuleni vichwa daima bz mtu bila nywele hajakamilika hahahahaaa....good day
ReplyDeleteKazi nzuri niile inayokuingizia pesa kwa faida,na uzuri salon zina risk ndogo mno hivyo ukiitwa kinyozi fajirika bz nikazi isiyo babaisha bz ufundi na matokeo huwa nipapo kwa papo sio akinawenzangu kasha kula hela kisha mzigo hajakamilisha. Ukiona MTU anaogopa kuitwa kinyozi ujue hajitambui yani haipendi kazi yake na akijidanganya kuwa ni mwelevu mno au kasoma sana basi ni msomi asiejitambua ktk eneo hili. Big up vinyozi kuleni vichwa daima bz mtu bila nywele hajakamilika hahahahaaa....good day
ReplyDelete