1.    Mhe. Balozi Begum K. Taj, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akiongea na baadhi ya wageni waliohudhuria maonyesho ya bidhaa za Tanzania
 1.    Mhe. Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji) akizungumza na Bw. Primus Kimaryo kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania;

 Wageni wakimsikiliza Mhe. Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji) akiongea wakati wa Investment Forum
 Mhe. Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji) akiongea wakati wa Investment Forum
 Baadhi ya bidhaa zilizoonyeshwa
 Baadhi ya bidhaa zilizoonyeshwa
 1.    Kikundi cha Utamaduni cha JKT Mgulani kilitangaza utamaduni wa Tanzania kwa kupitia nyimbo na ngoma za asili;
 Burudani yaendelea
 Mhe. Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Mhe. Balozi Begum K. Taj, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Marcel Escure, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania wakiimba na kucheza na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa.
 Mhe. Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii akiongea na mmoja wa wageni waliohudhuria shughuli hii
Khadija Mwanamboka alihudhuria shughuli hii na kutangaza utamaduni wa Tanzania kwa kupitia mitindo ya mavazi. PICHA ZOTE NA MIKE UDOFIA.


Ubalozi wa Tanzania mjini Paris kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania nchini Ufaransa waliandaa mkakati wa kuitangaza Tanzania hivi karibuni, ikiwa  ni sehemu ya pili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.  Sehemu ya kwanza ni tafrija iliyofanyika Desemba 2011 nyumbani kwa Balozi na iliwahusisha Watanzania tu.

            Mkakati wa kuitangaza Tanzania uligawanyika katika sehemu nne:-
Maonesho ya bidhaa za Tanzania kama vile kahawa, chai, konyagi, mvinyo, korosho asali, bidhaa za ngozi, khanga, vitenge, vinyago urembo wa kitamaduni, michoro (paintings) n.k., jukwa la kuelezea fursa za uwekezaji (investment forum) ambapo mada zilizotolewa na TIC, ZIPA, EPZA, NHC, Bodi ya Kahawa na OECD na  chakula cha jioni pamoja na onesho la mavazi  (Tanzania Mitindo House) na ngoma za utamaduni (JKT) pamoja na  maonesho maalum ya utalii (tourism road show).
Ujumbe wa Tanzania katika mkakati huu uliongozwa na mgeni rasmi Mhe. Dkt. Mary Nagu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji).  Wengine ni Mhe. Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. A. Shah, Mbunge wa Mafia, Mhe. K.S. Ole Telele Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Ali Seif, Mbunge toka Pemba, Mhe. D. Ntukamazina, Mbunge wa Ngara, Bi. Nakuala Senzia (TIC), Bi. Nana Mwanjisi na Bi Nasriya Nassor (ZIPA), Bi Zawadia J. Nanyaro (EPZA), Bw. William Genya na Bi. Susan S. Omari (NHC).

Wengine ni Bw. Pius Kimario (Bodi ya Kahawa), Bw. V. Laswai na Bw. Curthbet Sawe (Kibo Palace Hotel), Bi. Felista Rugambwa (Wizara ya Mambo ya Nje), Bi. Khadija Mwanamboka na Bi. Zamda Kiula (Tanzania Mitindo House), Kikundi cha Ngoma cha JKT kikiongozwa na Major Stanslaus Mishako.  Aidha wawalikishi wa TANAPA na Ngorongoro walihudhuria Tourism Road show.  Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Marcel Escure naye alishiriki katika mkakati wa kuitangaza Tanzania.
            Ubalozi unatoa shukrani za dhati kwa ujumbe uliotajwa hapo juu kwa kuhudhuria na kufanikisha mkakati huu.  Shukrani za pekee kwa waliochangia kwa hali na mali na kuwezesha shughuli yetu kufanikiwa nao ni:  Aga Khan Foundation kwa kutoa ukumbi wa kufanyia maonyesho ya bidhaa na jukwaa la fursa za uwekezaji Tanzania, Makampuni ya Tanzania: Uranium One, Quality Group na Tanganyika Wildlife Safaris (TAWISA) kwa michango yao ya fedha; Makampuni ya Ufaransa: Lafarge, Total, Shumberger na Thales kwa michango yao ya fedha na TANTRADE, Tanzania Distilleries na Tanzania Tea Blenders kwa michango yao ya bidhaa za Maonyesho.
UBALOZI WA TANZANIA
PARIS





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2012

    Nice...nimeona kitu cha Konyagi..my fav diamond..spirit of the nation.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...