Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Iddi Sanaly akiwa pamoja na Mhe. Balozi Mama Mwanaidi Sinare. Kwa wasioelewa maana ya DMV ni mkoa unaounganisha Washington DC, Maryland na  Virginia huko Marekani
Kutoka kushoto ni Bw. Charles Singili,  Mkurugenzi mkuu wa Azania BankCorp,  Bw. Oswald Urassa, mkurugenzi wa fedha wa Tanzania Mortgage Refinance Co. (TMRC ) na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar.
Kutoka kushoto ni  Bi. Nangi Massawe wa Benki kuu ya Tanzania,  Bw. Charles Singili wa Azania BankCorp  na Bw. Oswald Urassa wa TMRC
Rais wa Jumiya yaWatanzania DMV, Bw.  Iddi Sandaly,  akimkaribisha Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar kufungua mkutano huo.
Mhe. Balozi Mwanaidi Sinare  Maajar akifungua mkutano wa Maisha ni Nyumba uliofanyikia Mirage Hall jijini Washington DC, Marekani, siku ya Ijumaa June 1, 2012.
Mhe. Balozi akiendelea na ufunguzi huku wageni wa Maisha ni Nyumba na Viongozi wa Jumuiya wakimsikiliza.
Bw. Baracka Munisi akiwatambulisha viongozi wa Maisha ni Nyumba kwa Wanajumuiya wa DMV.
Bw. Oswald Urassa, ambaye ni Mkurugenzi wa fedha wa Tanzania Mortgage Refinance Co. (TMRC) akiongea .
Bw. Charles Singili, Mkurugenzi wa Azania BankCorp   akitoa ufafanuzi yakinifu  kwenye mkutano wa Maisha ni Nyumba uliofanyika Ijumaa June 1, 2012 kwenye ukumbi wa Mirage, Langley Park, Maryland.
Bw. Nehemiah Mchechu, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), akielezea mkikakati ya shirika hilo la kuwafanya Watanzania wawekeze katika ujenzi wa nhyumba
Bw. Rished Bade, Mkurugenzi mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Co. (TMRC) akifafanua jambo.
Bw. David Shambwe, Mkurugenzi wa biashara wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), akifafanua namna walio nje wanavyoweza kunufaika na mpango wa NHC na TMRC kujenga nyumba nyumbani Tanzania.


Pamoja na mvua kubwa kunyesha Ijumaa ya June 1, 2012 Watanzania walijitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa Maisha ni Nyumba uliofanyikia Mirage Hall, Langley Park, Maryland.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2012

    duh kweli mmejipanga hadi walioko mbele mmewatilia team-big up nhc

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2012

    Sasa huu mpango wa mortagage unawahusu walioko nje ya nchi tu? Mbona kina sie pangu pakavu hapa hapa nyumbani hatuufahamu vizuri? Kwenye website zenu hakuna maelezo ya kutosha kwani kungekuwa na maelezo ya kutosha yenye ufafanuzi mzuri msingekuwa na haja ya kufunga safari hadi nje kusaka wateja.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2012

    Nehemia Nchechu anafanya kazi nzuri ...............ombi langu ni kuwa watengeneze nyumba ambazo wengi wetu sisi makabwela tutaweza kununua kwa mikopo nafuu katia ya sh 20,000,000-50,000,000.
    Msiangalie tabaka la mabepari tu.

    Keep the good job.
    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2012

    mkurugenzi mpya una nia nzuri sana ila ninachotaka kusema ni kwamba kwa mfanyakazi wa kawaida sio rahisi kuweza kununua hizo nyumba zetu hata kama ni kwa mkopo kwa kuwa wafanyakazi hasa wa serikalini akimalia degree yake mshahara ni laki nne alikatwa katwa makodi anabakiwa na sh laki tatu na ushee sasa hiyo benki itamkopesha sh ngapi ili aweze kununua hiyo nyumba ya milioni 100 na ushee kama ilivyo nyumba nyingi mnavyozitangaza bei zake. ushauri wangu ni kwamba mngekuwa mnajenga hizo nyumba zetu nusu mngepangisha kwa bei ambayo wafanyakazi wa serikali wataiweza na kisha baadaye akiweza auziwe mtatusaidia kutokutoka usiku huku bunju kwetu muda mwingi wafanyakazi wanaupoteza barabarani. be advised pls

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...