Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza aliloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!
http://mnyika.blogspot.com/ 2012/06/msimamo-wangu-wa-sasa- juu-ya-kauli.html
John Mnyika
http://mnyika.blogspot.com/
John Mnyika
dOGO Mnyika namkubali kuwa ni mbunge mojawapo kati ya wachache wa upinzani ambao wana mchango mkubwa wa Taifa hili. huwezi linganisha na yule Lema anayejua kusema mbovu tu bila kuwa na mchango wa kibunge na wa kitaifa. ila kwa hili la leo mnyika amechemka, badala ya kujikita kutoa hoja ya kurekebisha mapungufu, yeye anamkosea adabu Rais Kikwete, ni kauli ambayo haiwezi kusimamisha bajeti kujadiliwa bali kuharibu tu hali ya hewa bungeni, sure, no positive inputs towards Tanzanian interests
ReplyDeleteSina chama chochote cha siasa ila huyu dogo nilikua namkubali kutokana na jinsi anavyowajibika na nafasi aliyopewa na wananchi ila kw akitendo alichokifanya jana Bungeni nimemtoa thamani.
ReplyDeleteWasiwasi wangu mkubwa ni kwamba hawa Chadema wakija kuchukua nchiitakuaje wakati mpaka sasa ambacho wao wameweza ku-prove kwa watanzania ni kwamba wamebobea kwenye lugha chafu. Tujiulize kipi ambacho Chadema mpaka sasa wameweza kufanya cha kudhihirisha kwamba wanaweza kuleta mabadiliko katika nchi.
Wananchi amkeni, hawa Chadema wapo ili na wao wapate fungu lao la kula pesa za walipa kodi maana wakibanana CCM itakua ulaji mdogo.
Mungu ibariki na isaidie Tanzania, AMIN.
Kaka umecheka katika hili....nenda taratibu umaarufu upo tu
ReplyDeleteHongera sana mnyika neno dhaifu wala si tusi sijui kwa upande wa wengine ila hata Yesu alisema hakuna aliye mkamilifu ila Mungu tu sasa watu wanapokuandama kuwa umetukana nashangaa sana. Lakini wala usivunjike moyo mi sina chama cha siasa ila nafatilia sana wale wanaopambana kutusaidia. Ulichosema ni UKWELI MTUPU HATA WAKATAE ILA HALI NDO HIYO KAMA NYUMBA INAYUMBA ALWAYS ANAANGALIWA BABA SASA KAMA NCHI IMEYUMBA NANI DHAIFU? ACHENI USHAMBA WA UVYAMA MUANGALIE MASLAHI YA NCHI. HAO WALIOTUKANA WENZAO KUWA VICHAA NA KUWA NA MAPEPO MBONA HAMKUWATOA NJE. MPINZANI AKIKOSOA MNASEMA KATUKANA FREEDOM IS COMING. HILI BUNGE ALIKUWA ANALIWEZA SITA TU THE GUY WAS REAL FAIR
ReplyDeleteBAJETI:
ReplyDeleteMapungufu ya Bajeti ukiyaangalia kwa makini haihitaji kuwa Daktari wa Uchumi ili kuona kuwa ina kasoro.
Muundo na Taswira ya Bajeti
A-Matumizi ya Maendeleo
B-Matumizi ya Kujikimu
Ni wazi kabisa inaonyesha kuwa zaidi ya 75% ya fedha zimeelekezwa kwenye kundi B wakati wakengwa ni Mabosi wa Mamlaka kwa Mishahara,Mafao na Vikao kwa kundi lao wakati walipaji wa gharama hizo ni kupitia kuwatoza Kodi Wananchi.
Hivyo Bajeti hiyo ipo nje ya Mpango wa Taifa wa kuwakwamua Wananchi dhidi ya ugumu wa maisha na sio kuchochea kupanda kwa ugumu wa maisha!
Kwa nini Bajeti hiyo isirekebishwe?
HAO CCM WAKITOA LUGHA CHAFU KWAO SAWA, MNAONA CHADEMA TU!!!!!!!TATIZO NI KWAMBA BUNGE HALIJATAMBUA MAANA YA UPINZANI, SIYO WOTE MNAONGEA LUGHA MOJA LAZIMA KUWEKO NA CHALLEGES.
ReplyDeleteHe should check how low his EQ is. He could have achieved the same effect with emotionally intelligent chosen words.Civility costs nothing.
ReplyDelete"Heshima kitu cha bure".
Dr Gangwe Bitozi.
wewe ni mbunge wa jimbo langu ila kwa ili la jana sio rafiki yangu inaonyesha ni jinsi gani hulivyokuwa huna heshima tukiondoa uraisi kikwete ni kama baba yako. kusema kweli umetuudhi wananchi hakuna hata mmoja ambaye anakuunga mkono wewe mnyika. kwa nini usiwe na lugha nzuri katika kuzungumza?
ReplyDeletenyie watoa maoni hapo juu msitulete udhaifu wenu hapa!tena mnyika hajasema yote kumwita rais dhaifu ni kosa?dhaifu ni tusi?matusi ni yale mawaziri wa ccm wanapokula billions of money za walalahoi na wanaviita vijisenti!dhaifu ni pale safari moja ya rais tena within africa inavyocost 3billions alafu wanasema zimeibiwa tumwiteje sasa?fikiria matatizo yakiyopo hapa nchini halafu mtu anaiba 3billion,ingepelekwa kijijini kwenu saivi ndugu zako wangekuwa na umeme na maji au hata shule wangevaa viatu.Acheni siasa kwenye mambo ya hela wazee maana hela ndo inaleta maendeleo.
ReplyDeletejamani kuweni basi na adabu kidogo siasa sio mdomo mchafu na matusi huyu raisi mmegeuza nani? ni juzi tu kule arusha yule arusha yule dogo kamporomoshea matusi ya kumwaga jamani naomba tuachieni huyu mheshimiwa. kama ninyi hamna heshima nae basi sisi tunamuheshimu.
ReplyDeleteAnonymos wote wa juu! Call a Spade spade and not a big Spoon! Acheni kujikomba! kwani udhaifu ni tusi? someone is weak ni tusi hilo au ni character? Think critcally, inatofauti gani na Kusema tunaogopa kufanya maamuzi ambayo kiongozi wa CCm aliwaambia bungeni siku moja Kuwa fanyeni maamuzi msiogope kufanya maamuzi?
ReplyDeleteWe Joni wacha utumbo wako! Wewe na Zitto mnajitia eti mnajua kila kitu. Eti nyinyi ndio wachumi stadi, wanajimu na ma-genius uchwara! Mbona hukuikosoa ilani yenu ya 2010 iliyodai eti kyadema mkipata madaraka mtatoa huduma ya afya 100% bure, elimu (chekechea mpaka kidatu cha sita) bure, mtauza vifaa vya ujenzi kwa bei ya chini kuliko ya gharama ya uzalishaji, mtapunguzi kodi zote bila kusema hizo shilingi trilioni 400 mtazipata wapi? Acheni danganya toto yenu! Mimi mchumi (BA econ. (hons)UDSM; MA Harvard, Mass. USA.)
ReplyDeleteKijana amekosa adabu ila mimi simlaumu yeye ila walezi wake!
ReplyDeleteMHESHMIWA MNYIKA KIDOGO PALE AMETUKWAZA WATANZANIA HUYU KIJANA NI MBUNGE AMBAYE SERIKALI YA TANZANIA INATAKIWA IMTUMZE SANA ANAWEZA KUINYANYUA NCHI NA KUIFIKISHA MAHALI PAZURI SANA KWA MAPUNGUFU HAYA ALIYOYAONESHA NI VEYMA BASI SERIKALI ITUMIE WAZEE WASHAURI WA HEKIMA KUMUELIMISHA NI JINSI GANI ANAWEZA KUCONTROL JAZIBA, BUSARA NA HEKIMA ZAKE ZINAWEZA KUNOLEWA NA ZIKAWA NZURI ZAIDI YA HAPO KWA MAUNGUFU ALIYOONYESHA BUNGENI ISIWE KIGEZO CHA KUONGEA MANENO AMBAYO YATAMVUNJA MOYO, HUYU KIJANA INGEKUWA ZAWADI YA CHEO ANGEPEWA UBUNGE WA AFRICA MASHARIKI ANGESIMAMIA MIKATABA VIZURI SANA KWA SABABU UPEO WAKE WA KUELEWA MAPUNGUFU NI MKUBWA SANA, MIMI PERSONAL NINGEOMBA SANA SERIKALI IMTUNZE NA KUMPA SUPPORT SANA HUYU KIJANA, PIA NAPENDA KUTOA POLE SANA MHESHMIWA RAIS KWA LUGA ILIYOUTUMIWA NA KIJANA NAOMBA MHESHMIWA RAIS ACHUKULIE TU NI KAMA KIJANA WAKE NA AMPENDE TU NA KUMPA MUONGOZO MZURI .
ReplyDeleteKIPEPEO
Kwa hali yeyote ile nilitegemea mbunge makini angejikita katika kutatua tatizo lililopo kwenye bajeti na kupatiwa walau ufumbuzi au kuona kuwa ametoa mchango kwa kufuata kanuni na taratibu zilizopo katika bunge.
ReplyDeleteNi kweli tulianza kusikia kauli mbalimbali zinazotolewa na wanasiasa kuwa bunge la bajeti 'litawaka moto' kwa maana tulitegemea kutakuwa na positive contributions na si haya maneno haya ya aibu.
Mungu ubariki Tanzania
Wabunge wanarushiana vijembe na kejeli bungeni, sasa dogo anamnanga Mkwere wetu wakati hayuko nae karibu ili kujibu mapigo.Mi naona amemkosea adabu Rais japo jamii ya kisasa kwao adabu, heshima, staha, uadilifu, unyenyekevu, uungwana ni msamiati. Zamani ilifundishwa kwa wazazi, walezi, skuli, jkt ...nk.Je tunawezaje kurudisha utamaduni wa maadili mema?
ReplyDeleteneno 'udhaifu' si tusi. Tena ni neno la kumkosoa mtu kistaarabu sana. Naona dogo hajakosea kabisa, unless kuna kipengele kwenye katiba kinachosema rais hakosolewi. Otherwise, namkubali sana huyu jamaa, tena kana akili kweli, na si kavivu ka kusoma mambo
ReplyDeleteHa haa, mmeona eeh, it is just a matter of time before people's true colours come out! we are watching!...
ReplyDeleteWewe ulosema una hons ya UDSM na masters ya harvard kweli hivyo vyuo sasa naona vimeporomoka kiasi kikubwa kama wewe unaweza changia kwa kiwango cha chekechekea make wa primary tu anakuzidi na hons yako. Mnyika nakupongeza saaaana wala usikate tamaa pambana tuko nyuma yako mimi nikirudi bongo nakuja kuchukua kadi na gwanda nataka pia. Angalieni mabunge ya ulaya wakubwa wanavochanwa na wala hawaanzi kubwabwaja eti wametukanwa. Rais ni mfanyakazi wetu kwahyo mfanyakazi yeyote anapokosea lazima umkanye kama ni mvivu nakadhalika tatizo lenu akili zimeganda kunyenyekea tu hata pale isipostahili. Hata baba akikosa unamwambia tu baba hapa umechemka kama ni muelewa tena atakushukuru na kuomba samahani, HONGERA SANA MNYIKA NAKUKUBALI SANAAAA. WATAALAMU WA KISWAHILI MTUSAIDIE KATI YA NENO KICHAA NA DHAIFU LIPI TUSI?
ReplyDeleteJamani watanzania tuache kuchochea vitu ambavyo vitatuvunjia amani yetu maana ilo suala la John neno udhaifu siyo tusi ni neno ambalo linaeleza mapungufu ya mtu, kwani kila mtu anamadhaifu au mapungufu yake no one is perfect in this world na linatumika sehemu nyingi. mfano mtu anaweza kukuuliza nieleze udhaifu/mapungufu wako/ yako ulipo ili nijue nianzie wapi kukusaidi ana kuwa ajakutukana au unaweza sema mimi ni mdhaifu wa hesabu unakuywa ujajitukana ila umeeleza wapi una tatizo. mimi ni mwana ccm ila kwenye suala kama ili siwezi kuweka uchama mbele. Michuzi halafu ubanie oni langu kama kawaida yako.
ReplyDelete