Neema Herbalist Co. LTD ni wauzaji wa dawa za asili..Kupitia mradi wetu wa ELIMU YA TIBA ASILIA KWA VITABU tunatangaza nafasi za kazi ya uwakala wa usambazaji vitabu vyetu kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani..
SIFA ZA WAOMBAJI.
1. Elimu kidato cha nne , sita na kuendelea.
2. Awe anaweza kuwasiliana kwa ufasaha kwa lugha za kiswahili na kiingereza.
3. Umri kuanzia miaka 18 hadi 35.
4. Awe maridadi, na mwenye uwezo wa kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa na kwa kujisimamia.
5. Akiwa na uzoefu na masuala ya usambazaji wa vitabu ama bidhaa yoyote litakuwa ni jambo litakalo muongezea nafasi ya kupata kazi katika mradi huu.
MAJUKUMU YA MAWAKALA : Kuchukua vitabu kutoka kwetu na kuvisambaza kwa wateja wetu waliopo katika eneo ama kituo cha kazi atakacho pangiwa na kampuni.
MALIPO KWA MAWAKALA :
Mawakala watalipwa " commission " nzuri.
IDADI YA MAWAKALA WANAOHITAJIKA :
Idadi ya mawakala wanao hitajika ni : Dar Es salaam ( 6 ), Mwanza ( 2 ) Arusha ( 2 ) Moshi ( 2 ) na wakala mmoja mmoja kutoka katika mikoa mingine ambayo haija orodheshwa.
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 22 June 2012..
Mawakala watakao chaguliwa watatangazwa tarehe 23 June 2012 na kuanza kazi rasmi tarehe 25 June 2012.
Kwa mawakala waliopo Dar Es salaam wanaweza kuleta maombi yao katika ofisi zetu zilizopo Changanyikeni karibu na Chuo Cha Takwimu.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Tuma barua yako ya maombi ya uwakala kwa njia ya barua pepe, kwenda : neemaherbalist@gmail.com . Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22 June 2012.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba : 0719 376 783 au 0752319341
Au tembelea blogu yetu : WWW.NEEMAHERBALIST.BLOGSPOT.COM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...