Hitima ya kuombea waliotangulia mbele ya haki na kuitakia heri na fanaka Yanga imekwishasomwa. Iliongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum. Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Omar Madega, Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi wa Julai 15, Clement Sanga walikuwapo. Sasa watu wanakula, Picha na BIN ZUBEIRY
 |
| Waungwana baada ya kisomo wakisubiri sadaka |
 |
| Sheikh Mussa kulia, kushoto ni Katibu wake Almasi lailly Mussa na nyuma yao ni mwanachama wa Yanga, Mustafa Mohamed, Katibu wa Tawi la Kurasini |
 |
| Madega kulia, akiwa na Sanga kushoto kwake |
 |
| Waungwana wakisubiri sadaka baada ya dua |
 |
| Katibu wa Yanga, Celestine Mwesigwa kulia, Madega na Sanga |
 |
| Sheikh Mussa katikati, kulia Juma Mnonji mwanachama wa Simba, na kushoto Katibu wake, Almasi |
 |
| Waungwana baada ya dua wakisubiri sadaka |
Maandalizi ya hitima katika klabu ya Yanga, makao makuu wa klabu, makutano ya mitaa ya twiga na Jangwani yanaendelea muda huu. Mboga zinakaribia kuiva, mchele umekwishaanza kuoshwa. Ng’ombe wawili wako jikoni. Ibada ya hitima yenyewe inakaribia kuanza kusomwa. Picha zote kwa msaada wa Blog ya BIN ZUBEIRY
 |
| Akina mama wakichambua mchele |
 |
| Akina mama wakichambua mchele |
 |
| Eneo la kusomea ibada ya hitima |
 |
| Waungwana tayari kwa kisomo cha hitima |
 |
| Mwanachama maarufu wa Simba, Mzee Juma Mnonji wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye hitima kama mmoja wa wageni waalikwa |
 |
| Masufuria jikoni |
 |
| Jamaa anatengeneza viungo |
 |
| Ng'ombe anaiva |
Hii Khitma ni ya nini mbona mie sijafaham (inasomwa kwa madhumuni gani), kulifiwa au kinakhitimishwa kitu gani, mana maelezo yake hayajajiweka wazi. Na hili sufuria la mwisho hapo chini linaweza kukufanya ukaisamehe karamu nzima na hamu yote ya kula ikakwishia, mana ukiliangalia lilivyo, halipo nadhifu kabisaaa!!!
ReplyDeleteMapishi ya chakula kwa staili hii ya mwaka 47 imepitwa na wakati. Makampuni ya kutayarisha chakula na kuleta kwenye shughuli yapo mwngi.
ReplyDeletembona hiyo sehemu ya kukatia vitunguu chafu jamani
ReplyDeleteSufuria kwenye picha ya mwisho linathibitisha udhaifu wa watani zetu...hapo hakuna hitima wala nini ni mambo ya siasa za mpira tu!! Yanga hakuna TIMU hata wakifanya hitima kila siku!!
ReplyDeleteHiyo sehemu ya kukatia vitunguu chafu jamani.
ReplyDeleteAnkal unatutia uchuuuu !
ReplyDeleteKwa nini usituwekee wakati ubwabwa umo ndani ya masinia na Waandazi wanayapitisha ktk safu za walaji unaowaita Waungwana huku yakiwa yamenona kwa minyama nyama?
Ingefaa ifanywe hivyo ili tumuumize Mwana Msimbazi mwalikwa kwa niaba ya wenzake huko Mzee Juma Mnonji, ili akasimulie kwa wenzake huko neema aliyoishuhudia iliyopo Yanga!
Je, Ubwabwa ni neema au siyo neema?
Au siyo?
Mjomba Michuzi umekosea kidogo!
ReplyDeleteUngetuonyesha na ubwabwa wenyewe ukiliwa kwenye masinia ili Simba waone neema tuliyo nayo sisi Yanga na kuwathibitishia hatuna njaa kama wao!
hv timu kama barcelona, arsenal, chelsea, manutd zinafanya huu upuuzi?kweli maendeleo tz itachukua karne
ReplyDeleteAssalama Lekko zake huyo aliyemleta Mwana Simba SC Mzee Juma Mnonji ktk Ubwabwa Yanga!
ReplyDeleteAnkal kwa nini usimpige picha huyo Mzee Juma Mnonji wakati akiwa anakuwa wali wetu?,,,tena wakati anapiga tonge na ananyofoa nyama?
Hata kama watamwelewa vibaya kula wali wetu Yanga ingesaidia kuwaonyesha Simba kuwa sisi Yanga unajua kuandaa Ubwabwa!
Ubwabwa wa Yanga:
ReplyDeleteWajameni Viwango vimezingatiwa kwanza?
Naona jamaa mkata viungo vitunguu picha ya pili kutoka chini ana plasta utosini, huku sufuria la nyama na mchuzi picha ya chini likiwa TBS imekwisha muda wake !!!
ngoja nipite zangu, Kama yanga mna utaratibu kama huu ambao ni mzuri sana si mnunue vyombo basi, hili sufuia la mwisho linatia aibu kwa club kubwa kama ninyi.
ReplyDeleteyanga kweli ni chama langu lakini jamani tuwe wakweli hili sufulia kweli kulikosekana masufulia ya maana mazuri na yakutosha maana chama kubwa alafu huduma mbovu mbona mnanifezehesha
ReplyDeletehilo sufulia utasema linalopikiwa supu uwanja wa fisi.
manji ana wamaliza wazee wa yanga kwa ubwabwa njaa jamani itatumaliza
ReplyDeleteWewe mdau wa kwanza, rudia tena kusoma hii habari taratibu. Mbona inaeleweka tu. Pia sufuria si tatizo. Kwani watu wanakula chakula kilichopikwa kwa sufuria hilo, lakini hawali sufuria
ReplyDeleteTuwe wakweli tu hata kama watu hawali sufuria ni wazi kwamba ni chafuuuu magonjwa mengine tunayatafuta wenyewe jamani kha! timu kubwa ivo mnashindwa kununua sufuria safi au kukodisha wapishi mahiri wenye vyombo vya kisasa?
ReplyDeleteUkimchunguza sana KUKU hauwezi kula nyama yake. Asiyeona wakati wa maandalizi ya kupika huu msosi atakula VIZURI tu kama chakula kitakuwa kitamu.
ReplyDeleteNimeamini timu za Tanzania zote ni za dini ya Kiislam, si unaona vikofia!!!! ha ha ha haaaaa....
ReplyDeleteJamaa anasema watu hawali sufuria jamaa yaelekea hata vyombo kwake haoshi kwani hali hayo masufuria sanakula cha ndani ya masufuria hahaaaÃ
ReplyDeleteMkata vitunguua mgonjwa ana donda utosini. Kapiga bonge la plasta na mabandeji. aaah mnatuangusha wana yanga wa huku mikoani, mnatunyima kauli kwa upuuzi kama huu. wapishi na majeraha ya vidonda.
ReplyDeleteJAMANI WATANZANI TUWEKE AFYA ZETU KWANZA MBELE, HUYO JAMAA ANAYETENGENEZA KACHUMBALI SIJUI SALAD , HUYO JAMAA SIO FIT KUWEPO JIKONI,YAANI HAFAI BINAFSI MIMI SIWEZI KULA CHAKULA ALICHOTENGENEZA BWANA HUYO ANAONEKANA NI DHAIFU NA HANA NGUVU KABISA MADONDA MPAKA KICHWANI, HAKUOSHA MIKONO WAKATI ANATENGENEZA CHAKULA HICHO HALAFU MARA WATU MNAUGUA ,MARA OOOH TUMEROGWA, NO HAKUNA USAFI HAPO . JE NA MAKAMPUNI YA UPISHI HAYAPO HUKO TANZANIA? NDIO YANGA KLABU KUBWA MNATEGEMEA KUCHUKUA USHINDI WA AFRIKA KATIKA HALI KAMA HIO?
ReplyDeleteNA HICHO SIO CHA KULA CHA MCHEZA MPIRA KAMWE HUO NI UROJO AU MNATAKA WACHEZAJI WAREGEE KAMA MDEBWEDO
Jamani mwandaaji wa kukata vitunguu ana plasta utosini na mabandeji!
ReplyDeleteHii mnajua kwa nini ?
Pale Yanga ni Mtaa wa Jangwani pana yale masuala ya 'maji ya betrii' na lile 'vumbi la kisasa' ,,,hivyo muda wote wapo bwiii kupigana mara kwa mara na misala kibao!
Bandugu Yanga Sports Club,
ReplyDeleteYaani hata kwa macho unaonekana huo mchuzi ndani ya sufuria la chini unaonekana upo chini ya kiwango cha ubora kabisa!
Ni wazi mchuzi kwake, vitunguu kwake, nyanya kwake huku nyama na marapurapu kwake!
Hivi kwa mtaji huo mtaweza kutufunga MSIMBAZI?
Hehehehe
ReplyDeleteWajameni Yanga Siposi Kilabu,,,hivi hiro risufuria na muchuzi huo hapo ndani ya risufuria ra chini ni wa kiwango cha magereza 'rupango' au ni wa uraiani?
Manake naona mchuzi umechambuka vipande vipande!,,,nyanya kwake, vitunguu kwake na mapira mapira ya manyama kwake!
Huu ni muchuzi wa Dona la Segerea Gerezani !!!
Hivi mudhamini wenyu Raisi wa Timu mutarajiwa Manji ingawa ndie aliyeandaa dishi ,je anaweza kula na nyinyi dishi hilo hapo?
Yanga mmefilisika!
ReplyDeleteEhhh mchuzi sufuria la chini unatoa povu?
Pana kila dalili nyanya za mchuzi huo hamkununua kwa fedha bali mmepewa za msaada!
Au nyanya mmepewa za masalo kutoka Sokoni Kariakoo?
Picha ya mchuzi sufuria la chini ni kuthibitisha ya kuwa Yanga ni timu ya Makuli wa kubeba mboga Sokoni Kariakoo!
ReplyDeleteHizo nyanya ni za mchango wa Makuli wa kubeba maguni ya mboga Sokoni Kariakoo!
Mnabisha?
Hahahahaha kweli Yanga kiboko sufuria ina fungus mwanzo mwisho.mkata kachumbari mkuu, ana donda la nguvu utosini pembeni yake kuna marapurapu ya nyama teh teh teh . Manji oyeeeee. ingekuwa Simba ndio inafanya hitma(kisomo) hiyo ingekuwa Sea Clif au Hyat yangekuwa yale mambo ya kujisevia kijiko kwa uma. Yanga mtasubiri sanaaaaa.
ReplyDeleteShukran uliyenirekebisha na kuniomba niipitie tena hii khabari. Nimeielewa vizuri sasa. Ila hilo sufuria bado ni tatizo japo umesema watu hawalili hilo sufuria, bali wala kilichopikiwa ndani yake. Ila hata kama jamani, usafi ni muhimu. Sufuria limefika kuraruka kwa shurba, mpaka limekuwa sugu kutakata, next time wasirejee kosa hili ni aibu.
ReplyDeleteJamani huyo mzee wa msimbazi asirudi msimbazi mpaka tumpime typhoid maana hiyo hali ya hapo hairizishi
ReplyDeleteMchuzi huo wa Yanga,
ReplyDeleteAchilia mbali hayo marapu rapu ya nyama,,,unafaa kunywa kwa kuzimua baada ya kulewa Gongo kali la matambara na mihogo!!!