Mratibu wa Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji miti ovyo na Uharibifu wa Misitu kwa nchi zinazoendelea (MKUHUMI) unaotekelezwa na Umoja wa Mataifa UN-REDD Bw. Ralf Ernst akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari yenye lengo la kujenga ufahamu miongoni mwao katika kuelekea kufanyika mkutano wa Maendeleo endelevu Rio+20 utakaofanyika kuanzia Juni 20-22 nchini Brazil kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kikundi cha Mazingira ambaye pia ndio Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Bi.Louise Chamberlain. Kulia ni Gertrude Lyatuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni "THE FUTURE WE WANT".
Bi.Gertrude Lyatuu (kulia) kutoka Umoja wa Mataifa akizungumzia mfumo wa uwezeshaji utakaopelekea uzalisha, usambazaji na matumizi ya bidhaa na huduma ikiwa ni matokeo ya kuboresha maisha ya mwanadamu kwa muda mrefu kwa kutunza mazingira bila kukiangamiza kizazi kijacho.
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro akizungumza kuhusu umuhimu wa mkutano wa Rio+20 na maana yake katika kuipeleka dunia pale inapotaka kwenda. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na kushoto ni Aifsa Mkuu wa Utafiti wa Masuala ya Mazingira katika Ofisi hiyo Dkt. Constantine Shayo.
Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi (hayupo pichani).
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akifafanua kuwa Tanzania kama mwanachama wa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi amesema Tanzania imeandaa Rasimu ya Ripoti ya Rio+20 itakayojadiliwa na mkutano huo.Bw. Muyungi alitumia fursa hiyo kuwakilisha mada kuhusiana na maendeleo endelevu ya Tanzania katika miaka 20 tangu mwaka wa kwanza kufanyika mkutano wa kwanza wa RIO iliyohusu "wapi tulipokuwa na wapi tulipo sasa".Bw. Muyungi ameongeza kusema kuwa Mkutano huu utaainisha hatua zitakazoangalia utekelezaji na kuhuisha nguzo zote tatu za maendeleo endelevu (mazingira Uchumi na Jamii) kwa kufuata kanuni za usawa huku tukitambua tofauti katika uwajibikaji na uwezo.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini walioshiriki warsha iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mtaifa kuhusiana na Umuhimu wa kufahamu na kutunza mazingira ikiwa ni katika Siku ya kuadhimisha Mazingira Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini walioshiriki warsha iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mtaifa kuhusiana na Umuhimu wa kufahamu na kutunza mazingira ikiwa ni katika Siku ya kuadhimisha Mazingira Duniani ambapo kitaifa imefanyika mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2012

    Swala la mazingira ni Muhimu sana kwetu sote. Pamoja na semina na warsha na makongamano yoooote haya yenye kugharimu pesa mingi sana bado wadau - washiriki huishia kulamba allowances na kuishia kunako mishe mishe nyingine! Wapo wachache wenye kurejea kwa jamii na kutekeleza maazimio na makubaliano-Honera- Jamii tujue kutunza mazingira. Serikali na halmashauri ziwe za kwanza kuratibu kutekeleza na kutunza daima mazingira tukianza na kusafisha maeneo ya miji yetu, kuapnda miti na maua mazuri na kuvitunza!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2012

    Hongera Manispaa ya Moshi kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira Kitaifa. Pamoja na kazi nzuri mnayofanya - wawepo wadau wa kuboresha maeneo kwa - Land scaping km Eneo la YMCA Round about hususan sehemu wapita kwa miguu kuna vikorongo vya hatari - vyaweza kujazwa kifusi na kusawazishwa vikawafaa sana watembea kwa miguu. Barabara iingiayo mjini yaweza boreshwa kwa landscaping nzuri - ukoka na maua mazuri na walkways nzuri pakapendeza. Kwa ushuru mnaokusanya Inawezekana! Bado yapo maeneo mengi kama hayo yanayoweza kuboreshwa zaidi. Together we can make it Hongera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...