Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar


 VIONGOZI wengine wawili wa Jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, wamefika Makao Makuu ya Upelelezi Zanzibar ambako walihojiwa kwa muda kuhusiana na vurugu za wiki iliyopita visiwani hapa kabla ya kuachiliwa.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amewataja Viongozi waliofika Polisi na kuhojiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamshio Shekhe Mselem Bin Ali, mkazi wa Makadara na Shekhe Azan Ahmed Saidi, wa Mfenesini.

Inspekta Mhina amesema katika mahojiano hayo Polisi walibaini kuwa siku ya vurugu hizo, viongozi hao hawakuwepo mjini Zanzibar ingawa Polisi walitaka kujua zaidi kama wao walihusika katika maandalizi ya awali ya mpango huo kabla ya kuondoka kisiwani hapa.

Wakati wa matukio hayo Sheikhe Mselem alikuwa Pemba na Shekhe Azan alikuwa Uwarabuni kwa matibabu lakini alilazimika kurejea Zanzibar baada ya kusikia hali ya vurugu zilizofanywa na vijana wa kikundi chake.

Viongozi hao wanafanya idadi ya viongozi waandamizi wa Jumuiya hiyo waliojisalimisha na kuhojiwa kwa hiyari na Makachero wa Jeshi la Polisi mjini Zanzibar kufikia sita.

Jana viongozi wengine wanne kutoka katika kundi hilo la Uamsho, walijisalimisha wenyewe Polisi na kuhojiwa kwa masaa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa masharti.

Inspekta Mhina amesema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa viongozi wengine wa Jumuiya hiyo ambao hawajafika Polisi, kufanya hivyo badala ya kusakwa na kutiwa nguvuni kuhusiana na vurugu hizo.

Wiki iliyopita Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, walifika mjini Zanzibar na kuwataka wale wote waliohusika katika vurugu hizo kujitokeza kukabili mkono wa sheria.

Tayari watu 78 wamekamatwa na Polisi na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya vurugu zilizosababisha kuchomwa moto kwa magari na baadhi ya makanisa mjini Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2012

    Masheikh:

    Mashariti ya ziada baada ya kujisalimisha kuhojiwa na kuachiliwa na Idara ya Usalama na Polisi ni kuwa muendeshe Madrassa kwa Vijana wenu wa Kundi la Uamsho ili wailelewe vema Dini ya Kiislamu ambayo vitendo walivyofanya haviendani kabisa na Itikadi ya Kiimani ya Kiislamu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2012

    Inaelekea kama vile mna walea hawa hamko serious na hili jambo. Vurugu lote na kusababisha uharibifu mkubwa, uvunjifu wa amani na ubaguzi wa kidini kwa kuchoma makanisa mna wabembeleza hawa? Wahujumu wa amani ya nchi sio wa tu wa kucheka nao ni maadui wakubwa kulikoni adui mwingine ndani ya nchi, Please please be serious and take very strong measures against this caliprits.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2012

    Hizi zama naona ni za mwisho!Watu wanafanya uharifu kwa kisingizio cha Dini ya Kiislam,,Hata kama mtu unataka haki yako,,iombe kwa utaratibu sio kuibia watu au kuvunja makanisa,,au hata kuuwa,,Inasikitisha sana kuona sisi waislam tunauwana kama wanyama,,hasa huko Syria,watu jamani wanazikwa kimfereji kwa ajiri ya wingi wa watu waliouwawa bila hatiya

    Mimi mwenyewe binafsi napenda tuendelee kuwa pamoja na wazenj,,ila ni kweli kama kuna kitu wanaonewa kiuchumi au kiuongozi ama Kitaifa upatikane muafaka wapewe haki yao,,kwani ni nchi nyingi Duniani wameungana lakini kila nchi ina haki yake,,

    Kama ni kuhusu uchumi au misaada,hata sisi wenyewe Bara tuko hoi bin ta'abaan,nchi wanaifaidi wachache,,msione tuko kimya tu,,tunakufa kiofisa na tai shingoni,,,,
    KUWEPO KWA MUUNGANO NA HASA SISI WAISLAM WA BARA KUNATUPA FARAJA A BIT,,Mkijitenga NDUGU ZETU NIKAMA MNATUTUPA,,(Uzalendo unakuwa umewashinda),,,
    Kikundi hikicha Uamsho!Vingozi rudini katika vitabu na Hadith za Mtume wetu Muhammad S.A.W ili mfanye kitu hiki kwa njia ya Kiislam,,Inawezekana kweli hamkushiriki katika mambo hayo wala hamkuandaa chochote katika vurugu hizi lakini mnakuja kubeba mzigo wa lawama na Dhambi kwa kuwepo kikundi hiki au kukianzisha,,na inatokana na mawaidha mnayo wapa vijana wenu ni ya namna gani.

    Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania na Dunia nzima kwa Ujumla!..'Amiin Rabil Alamiin'

    Ahlam,,London

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2012

    Laiti wangekuwepo wale viongozi wenye uchungu na nchi na kuthamini uhuru na utu, hicho kikundi kisingefikia hata kuandikwa gazetini. Utwana mbaya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2012

    'Not guilty until proven guilty' ni nani aliewaona vijana wa muamsho wakifanya uhalifu huo,au leo munataka kusema kuwa vijana wu muamsho ni wanywa pombe ? kwa maana walionekana kati ya hao wliovunja bar wakinywa pombe hadharani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2012

    WaTanzania kwa kuhukumu kabla ya Mahakama wamezidi! Hata ishu ya Lulu, walishamhukumu kabla ya Mahakama!

    Be educated and civilised.

    Mwenye uwezo na mamlaka ya kusema iwapo Uamsho walihusika na uchomaji moto wa makanisa, ni MAHAKAMA tu, na si vinginevyo!

    No evidence, no right to speak!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2012

    KUNYA ANYE KUKU AKINYA BATA KAHARISHA

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 06, 2012

    Mchanhiaji wa mwisho acha umbumbumbu.Kwani waliofanya fujo wako wazi ni wa junuiya hiyo ww unataka ushahidi gani ilhali hata viongozi wao walikiri kuwa walitenda na wataendelea kudai haki yao,wakasema kama wakichokozwa wataendelea kujibu mashambulizi.Wao wanasubiri wasumbuliwe na kina nani ilhali wao ndo wasumbufu mafisadi wa amani?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 06, 2012

    hao ni kuwaweka ndani tu, mnawaachia wa nini?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 06, 2012

    Tusitetee uharamia. eti mpakaithibitishweje manake mioto iliwaka na mali kuharibiwa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...