Mh. Alhaji. Adam Kimbisa

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hilo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose Saddrudin Bhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapishwa pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mh. Shy Rose Banji .
 
Mh. Samuel Sitta ni muwakilishi wa Tanzania 
Mh. Abdullah Alli Hassan Mwinyi 
Mh. Charles Makongoro Nyerere
Mh. Dkt. Twaha Issa Taslima
Mh. Nderkindo Perpetua Kessy
Mh. Bernard Musomi Murunyana
Mhe. Anjela Charless Kizigha


Picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2012

    Hivi Mhe. Shyrose anaapa kwa kutumia kitabu gani maana naona ni tofauti na vingine walivyoshika waislamu na wakristo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2012

    Quran ile mheshimiwa au umeonaje?labda macho yangu huenda ikawa ni kitaku cha ujamaa ukoministi kisochoamini dini yeyote

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2012

    SHY ROSE YEYE NDO KAONYESHA DHAHIRI SHAHIR (WAZI WAZI) KWAMBA NI MTOTO WA KIISLAMU KILA ALIYE NA MACHO KAIONA ILE QURAN YENYEWE SIYO WENZAKE WAMEIFICHA MKUU HAPO JUU ULIYETOA COMMENT HUONI BWANA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2012

    Imani zipo nyingi....usikariri mdau

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2012

    mkuu unaesema kuwa shy rose ndio alieonyesha dhahir shahid,umeangalia kweli alichokishika? ameshika kitabu cha tafsiri ya Quran sio msahafu. Sisemi shy rose sio muislamu ila nasema alichoshika sio mshahafu mtukufu ila ameshika tafsiri ya mshahafu, kuna tafauti kubwa hapo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2012

    Hiyo Ni AL FURQAAN au QURAAN TAKATIFU:

    Inshallah Mwenyezi Mungu wa Rehma amzidishie!!!

    Hakuna ubishi Shyrose Bhanji ni Binti wa Kiislamu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 06, 2012

    Ile ni Quran,

    Shyrose ni Mwislamu, msije mkababaika na hiyo ROSE mwisho ktk jina lake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...