Wakali Dancer wakiwa na bendera yenye nembo yao wakati wakisherehekea miaka 4 ya kuanzishwa kundi lao.
Kundi la Wakali Dancers likishambulia jukwaa.
...wakizidi kunogesha sherehe hizo.
...wakicheza wimbo wa Thriller ulioimbwa na Michael Jackson.
...wakizidi kupagawisha.
Wanamuziki wa Kings Taarab wakiwa jukwaaani.
Maua Tego wa Coast Taarab akiwajibika.
Talent Band wakitoa burudani kwa mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka.
Wakali Dancers wakipongezwa.
Familia ya mmoja wa wasanii wa Wakali Dancers ikifuatilia onyesho hilo.
Kundi la Kidumbaki likitoa burudani.
Msanii wa Kidumbaki akionyesha maujanja.
Msanii anayefahamika kwa jina la Zimwi akitoa burudani.
Mpigapicha mahiri wa magazeti ya Global Publishers, Issa Mnally, akilishwa keki na shabiki wa burudani.
Mmoja wa wawakilishi wa Wakali Dancers akilishwa keki ya Jumapili.

SHEREHE za miaka minne ya kundi la Wakali Dancers jana zilifana ndani ya ukumbi wa kisasa wa burudani, Dar Live uliopo Mbagala Zakheem, jijini Dar. Vikundi vya taarab vya Kings, Coast Modern na Kidumbaki kutoka Zanzibar pamoja na Talent Band vilifanya ‘bonge la kufuru’ kwa mashabiki waliofika katika ukumbi huo kwa ajili ya kuburudika wikiendi. Picha zote na Global Publishers 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kumbe wana 'KIDUMBAK' nao hawapo tiro! Si ajabu next time tukasikia na BENI nalo likiunguruma ndani ya Dar Live.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2012

    Kidumbaki nimeipenda sana, ntapata wapi video yao. Mimi napendaga kuona vya kwetu pia. Haya mautamaduni ya kigeni ishakuwa tuu mach.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2012

    Anon. wa pili ingia youtube utakuta mpaka MSEWE huko pitia uchochoro huu http://www.youtube.com/watch?v=h5ncGpjKmVU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...