Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Chocky akiimba katika moja ya shoo walizoanza kuzifanya nchini Finland wakati wa Tamasha la First Afrika.
Kiongozi wa wacheza shoo, Super Nyamwela akicheza sambamba na wacheza shoo wenzake Finland
Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo wakicheza wakati wa tamasha hilo nchini Finland
Kiongozi wa Wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo, Super Nyamwela akiwaongoza wazungu kucheza baada ya kuvutiwa na staili za wacheza shoo wa bendi hiyo.
Wacheza shoo wa Extra Bongo wakicheza huku wakiwa kwenye vazi la asili ya Kitanzani nchini Finland kwenye Tamasha la Fist Afrika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    KWANINI PICHA ZA ULAYA HUWA AUDIENCE HAIPIGWI PICHA WANAOPIGWA PICHA NI WALE WALIO JUKWAANI WAKATI NYUMBANI KUNDI LA WATU WALIOHUDHURIA HUPIGWA PICHA, HII INAONYESHA PICHA ZINAPIGWA KISIASA NA UKUTE MAHUDHURIO SI MAZURI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    huku ulaya sheria inachukua mkondo endapo utampiga picha mtu na kuitundika mtandaoni bila ridhaa yake. hivyo wengi hawapendelea kutoa picha ambazo sura za watazamaji/washangiliaji zinaonekana. hili ni suala zima la PRIVACY ya mtu binafsi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    Privacy kitu gani? Acha kutufanya wapumbavu. Kawadanganye huko nyumbani Tanzania .

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2012

    Mmmh we anony Mon Jul 23, 12:11:00 AM 2012 ebu tuheshimiane. Mara ngapi tumeona sura za watu kwenye concert za kina Elton John? tena mtu anafanywa kuvutwa kwa karibu kabisa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2012

    Anony wa pili: ni muongo heti ulaya sheria hairuhusu kupigwa picha audience sio kweli kabisa ,ulaya wana freedom of the speech and press,ndio maana mapaparazi wanatajirika kwa kupiga picha za mastaa na audience,kilichofanyika katika picha hizi ni kuwapiga wasanii kuliko audience

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2012

    wewe wa pili hapo, huna hata haya !! eti privacy na eti huku Ulaya sheria inafuata mkondo wake !!! wewe limbukeni nini ?? Michael Jackson akiwa jukwaani na huo umati tunaouna na wengine wanazilai AU Madona akiwa stajini ???? kwani lazima u comment ??? hata kama hujui kitu !!! aaaa !!! hawa watu walioko majuu, siyo wote lakini naona wengi wao ni darasa la 7, sasa walipofika kule , wanadandia mambo bila elimu. Je na huko kwenye viwanja vya mipira nako-mbona mashabiki wanaonyeshwa sura zao,au labda wapiga picha huwa kwanza wanawataka radhi ???? stop the nonsense and get real. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2012

    MDAU MTOA MAONI WA KWANZA HAPO JUU HEBU NENDA KASOME DARASA LA ANKAL KUHUSU UPIGAJI WA PICHA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2012

    Tumewekewa picha za Extra Bongo wakiwa stejini Ulaya. Sasa ulitaka mashabiki wa nini? Wewe mashabiki wanakuhusu nini? Au unahisi umedanganywa hapo ni Chalinze na si Finland? Tuwe tunafikiri kabla hatujaibua mjadala wajameni...

    Ramadhan kareem....

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2012

    Mahudhuria yalikuwa mazuri kwa hilo ondoa hofu.


    Na kazi waliyopiga jukwaani ilikuwa kubwa sana wakiwa na wasanii wenye ubunifu wa hali ya juu.
    Kama unapenda kutazama wahudhuriaji unaweza kubofya hiyo link utakidhi kiu yako
    http://edondaki.blogspot.fi/

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...