Hivi ndivyo hali inavyokuwa hasa wakati wa Jioni wakati magari makubwa yakiwa katika foleni ya kuelekea kupima uzito kwenye Mizani ya Kibaha mkoani Pwani,ambapo kutokana na kwamba kuna magari mengine hayatakiwi kupita kwenye mizani hiyo hivyo yanalazimika kuyapita magari hayo yaliyo kwenye foleni ili kuendelea na safari zao.sasa wahati mwingine mambo huwa namna hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    kwa nini mmekuwa watu wakushindwa kufikiria hata namna ya kupanga magari barabarani??

    msaidiweje sasa kuku nyie??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2012

    Panueni barabara kwa umbali mrefu ili gari zinazopaswa kupimwa uzito zianze kuiacha main road mapema zaidi.Na ikiwezekana kuwe na mizani 2 au 3 katika eneo hilo kuharakisha mambo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2012

    Wakati mwingine wenye mamlaka utendaji wao ni hafifu lakini hakuna anayeulizwa wala kuongezewa uwezo ili akiendelea na makosa apishe wenye uwezo wa kiutendaji, ubunifu na kujituma. Hapa magari yakisimamiwa vema kunakuwa hakuna foleni mimi ni mkazi wa Kibaha nimeshuhudia. Wanapokuwa watendaji wazembe kwenye zamu hali hii hujitokeza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2012

    Fikiria kunagonjwa mahututi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2012

    Mdau wa Mon Jul 16, 05:02:00 PM 2012 kwa sasa hiyo ndo njia sahihi ya kupunguza msongamano. Mbali na hizo jamaa walishatengeneza mizani pale Mikese na huku mbele ya Chalinze tena ipo miwili lengo ni kupunguza foleni kwa magari yatakayokua yakija Dar yasipite Mizani ya kibaha tena. Juhudi wameshafanya sema ndo hivyo gari za mizigo nazo zinaongezeka kila kukicha .So kuna haja ya kuwekeza kwa kuangalia miaka 20 ijayo ukizingatia ongezeko la maroli kwa kipindi cha miaka 8 iliyopita

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2012

    Hiyo mizani ingetolewa hapo ipelekwe mlandizi huko eneo kubwa tu , uvivu tu wa kufikiri Kuku wa kienyeji nyie !!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2012

    Kupima mabasi ni kuongeza usumbufu kama tunaouona hapa. Tanzania ni nchi pekee Afrika inayolazimisha mabasi kupimwa katika mizani. Ni malori yaliyopakia mzigo kupita kiasi yanayoharibu barabara, si mabasi. Na huyo aliyesema mizani iondolewe hapo namuunga mkono kwa asilimia 100. Sehemu hiyo ni finyu. Mizani ipelekwe kati ya Mlandizi na daraja la reli la Ruvu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...