Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(wa tano kushoto) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar,swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,(katikati) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya Waislamu waliohudhuria katika Hitma ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul,iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameungana na viongozi mbali mbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar.

Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar-es-Salaam kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa.

Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk. Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Mhe. Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri,Wabunge,Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. "ALLAHU MAGH'FIRLAHUM WAAR'HAMAHUM WAASKANAHUM MAKANA FIL'JANNAT' N'NAEEM") - AMEEN AMEEN YAA RAB'BAL-ALAMEEN.

    Na tuwe pole watanzania wote kwa jumla khasa ndugu zetu wa Visiwani na wote waliofikwa na kuguswa na msiba huu, khususan waliowapoteza ndugu zao, jamaa na marafiki. Wao wametangulia nasi sote tupo nyuma yao na kwake (MOLA) tutarejea.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2012

    Mtasoma sana hizi hitima za namna hii kama hamna badilika na kuanza kutibu mizizi badala ya kutibu matawi.we have long way to go.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2012

    Wabongo kila kitu tunafanya hovyo, mfano kupandia madirishani, kutanua, kujisaia nje ya tundu, lugha chafu,....yaani, hata Mungu keshatuchoka kwa unafiq wetu wakati sisi wenyewe ndio wapuuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...