Ndugu Wananchi,

          Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. 
Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. 


Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa madaktari.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2012

    Maelezo mazuri kutoka upande wa serikali. Lakini ili tutende haki katika kujadili, tunaomba Chama cha Madaktari na jumuia zake nao watuekee makubaliano yako kwenye blog hii ili tuweze kutoa maoni yetu sisi wananchi katika suala hili la mgomo.

    Lakini haya yalioandikwa ndivyo yalivyo, tunawashauri madaktari warejee kazini kutuhudumia sisi wanyonge, serikali imejitahidi sana.

    Sitegemei kama madaktari wao katika meza ya mazungumzo wategemee yao tuuu ndio yakubaliwe.

    Kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais, serikali zetu za dunia ya tatu, ni vigumu kutekeleza hayo madai kwa wakati mmoja. Lakini hili pia tunaweza kulichukulia katika familia zetu, si kila kitu tunachokihitaji kunakitimiza wakati uo huo.

    Mazingira kuboreshwa ni mipango endelevu tena ya muda mrefu. Si rahisi, kutoka March hadi June, wodi za akina mama kwa mfano ziwe zimejengwa nchi zima ili wasilale chini au zaidi ya mmoja kitandani!! Kwa hili tuwe wakweli jamani.

    Mwisho naomba madaktari wenzangu, tuwe na huruma kwa jamii tunayo humia, kwa kweli inahitaji huduma yako. Kilio chenu kimesikika kwetu wananchi. Muda upo wa kuyahoji haya kama yatapuuzwa. Si kulazimisha kila jambo lazima litekelezwe wakati uo huo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2012

    Pongezi kwa rais kwa ufasaha na hatua zilizochukuliwa na serikari mpaka hapa. KI MSINGI HATUHITAJI MAELEZO MENGINE KAMA RAIS WA NCHI KISHASEMA.
    ASIYETA MSHAHARA WA SERIKARI NA MARUPURUPU MADOGO YA SERIKARI NA AONDOKE AKAFANYE ATAKAPOPATA MARUPURUPU BORA. UGOMVI WA NINI TENA
    PILI NAOMBA MHESHIMIWA KWA UPANDE WA SERIKALI MAJADIRIANO KUHUSU HILI YAFUNGWE, INATOSHA SASA NA TUFANYE KAZI.
    NAOMBA MADAKTARI WOTE WALIOGOMA WAFUKUZWE KATIKA MUDA USIOZIDI MASAA 24 BAADA YA HOTUBA YA RAIS.
    TAFADHALI WARUDISHE NA KUHAMA NYUMBA ZA SERIKALI MARA MOJA.
    MH. RAIS KWA NINI UMEKUWA NA HURUMA VIVYO HATA KWA ANAYEVUNJA SHERIA ? NA WEWE ULIAPISHWA KULINDA NA KUTETEA SHERIA NA HAKI
    MBONA HAKI YETU YA KUTIBIWA MADAKTARI WANATUDHULUMU NA WEWE MTETEZI WETU UPO ?
    MH. RAIS CHUKUA HATUA KALI KWA YEYOTE ANAYEVUNJA SHERIA NA HASA KWA HAWA MADAKTARI NA SISI WANANCHI TUNAKUAHIDI USHIRIKIANA, TUKO PAMOJA NA WEWE RAIS WETU. WANATUNYANYASA MNO, WANATUTESA NA WANATUUWA HAWA SI MADAKTARI KIIMANI BALI NI WATAKA FEDHA TU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2012

    Mh Rais katoa kauli na iwe ya mwisho.Madaktari warudi kazini kama hawataki wakafungue hospitali zao.Ila pia wanasiasa waache kujipendelea kwani kwa kiwango kikubwa ndo wanasababisha confrict na wataalamu pale wanapojipangia mapesa mengi wakati wataalamu wetu wakiumia. Haiingii akilini kwa posho za wabunge wetu na posho ya daktari aliyokuwa anapata ya sh 10,000/=

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2012

    Hongera mh. Rais kwani wenye macho wameona na wenye masikio wamesikia! Huruma yako ndio inayosababisha yote haya kwani kwa hesabu hizi sifikiri kama walipaswa kugoma labda watuambie kama walikuwa na agenda nyingine!hawa madaktari wasio na na wenye tamaa ya fisi na wauwaji na kama alivyosema JK yanini kama unions maslahi madogo Kula kona kwani tumeshawazoea kukimbilia Botswana, Zimbabwe na kwengine!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2012

    mimi nanshukuru sana Raisi kwa maelezo mazuri aliyo toa, kiukweli labda sio mapendekezo yote ya madaktari yanaweza kutimizwa hivi sasa, ila swali ni kwamba nili sikia posho ya postportum imeongezwa, hopo ndio tunaangalia vipaumbele ni vipi? huwezi anza ongeza posho ya kuchunguza maiti wakati bado hela zinahitajika kulinda afya ya aliye hai. pia kwa wanao sema daktari wanatuua, mimi navyodhani mimi kama mwananchi ni jukumu la serikali na daktari ni mfanyakazi wa serikali, sasa pale dkati na serikali ambao ndo majili wake wakishindwa kuelewana ana daktari akakataa kufanya kazi wa kumlaumu ni muajili kwanii hafikii maelewano na mfanya kazi wake ili mimi mwanannchi nipate huduma, ila yeye ananishtakia mimi kua alie mwajili amegoma sasa mimi ntafanya nini? na wakati kama huo inchi inasema haina fedha mbona wamepata billion mia mbili kwa wiki kwaajili ya kukodi madaktari nje, basi kuna hela ipo ambayo haina kazi. kama daktari asingegoma hiyo billion miambili ilikua inaenda kufanya kazi wapi kama sio mifukoni kwa watu[viongozi]?
    mimi mambo mengi yananichanganya kuhusu hii serikali hadi sijui niwe upande upi?.
    ukiwaza mwalimu analipwa laki moja na sabini kwa mwezi wakati mbunge anapewa posho ya laki tatu kwa siku, sasa kama mwalimu anajibana anatumia laki moja kwa mwezi mbunge anatumiaje hela hadi ila elfu sabini ilikua haimtoshai hadi imeongezwa kuwa laki tatu??? akigoma mwalimu tutaanza tena kusema walimu wamezidi kugoma, wagoma kwasababu haiwaingii akilini kua mbunge analipwa hiyo hela na mfanyakazi wa TRA analipwa mamilion afu, unasema wanalipwa sana kwasababu wao sio wafanya kazi wa umma.
    wote wanafanya kazi kwaajili ya nnchi, sasa wenye kazi ngumu na mazingira magumu ndo wanao lipwa kidogo ila aliekaa ofisini kwenye kiyoyozi ndo anaelipwa sana. sio haki kwakweli mgawanyo wa fedha unahitajika ili kila mtu afanye kazi yake kwa amani na uaminifu.
    Raisi anasema madaktari ambao hawataki wahame nnchi, sawa wahame ila swali ni moja, madaktari tulionao wako kwenye ratio ya zaidi ya 60:1, na hii mepatikana baada ya miaka 50 ya uhuru, wakiondoka ili kuja kupata idadi nyingina kama hii itatughalimu sio chini ya miaka 25 mingine mbele, sasa tunajenga au tunabomoa???
    na kama wakija hao wa kukidi naona kama ghalama zitazidi mishahara ya madaktari ya sasa mara 10 hivi, mimi siomi pointi hapo hata kidogo.nina mengi ila ngoja niishie hapa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2012

    Hongera sana mheshiwa Rais, sisi tumekuelewa, asiyekuelewa huyo haihitaji kuelezwa zaidi ya hayo, hiki ndicho tunachihitaji kusikia, na nakupongeza sasa kwa uamuzi wa kuongea nasi mojo kwa moja kulikoni ile ya kuongea na wazee, tulikuwa tunaona kama unatupiga vijembe, big Up
    ndugu zangu madaktari naamini mnasoma maoni yetu, tunaomba mrudi kazini, Naamini wote mna dini, kama sio wakristo ni waislam, na vitabu vyetu vya dini vinaongerea kuheshimu mamlaka, na mamlaka ni serikali yetu, Tuiheshimu, hii amani tunaichezea tutakuja kuikumbuka. tunakuombea Mh Raisi katika uongozi wako, lakini tujitahidi kutatua matatizo wa watumishi na mungu akuongezo katika kutatua matatizo hayo,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...