Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, (NUU) Mhe. Edward Lowassa( Mb) akiwa na Kaibu Balozi wa Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe.Lowassa akiwa na wabunge wanne wamekamilisha ziara yao ya kikazi na mafunzo, ziara ambayo ilikuwa na lengo la kujionea hali ya utendaji kazi katika vituo vya Ubalozi nchi za nje, kujua mafanikio, matatizo na changamoto wanazokabiliana nazo watendaji, ikiwa ni pamoja na namna ya kutafuta njia bora zaidi za kuimarisha utendaji wa kazi ili uwe wenye tija zaidi. Aidha Kamati hiyo ilipata fursa pia ya kutembelea na kukagua mali zinazomilikiwa na serikali hususani majengo.

Na Mwandishi Maalum.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ( NUU) Mhe. Edward Lowassa (Mb), amewaasa Maafisa wa Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, kutotetereka wala kuyumba pale inapowapasa kutoa misimamo kwa maslahi ya nchi yao.

Ametoa wasia huo wakati alipokuwa akitoa majumuisho ya ziara ya kamati yake, ziara ambayo pamoja na mambo mengine ililenga kujifunza na kujionea hali hali ya mazingira ya utendaji kazi ya maafisa wanaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Akimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mhe. Lowassa alikuwa na haya ya kusema.

“ Mwalimu aliwahi kutueleza huko nyuma kwamba, jambo linaloipa heshima kubwa Tanzania licha ya umaskini wake ni namna isivyotetereka katika kukisema na kukitetea kile inachokiamini hata kama kinawaudhi wakubwa. Kwa hiyo nami ninapenda kwanza, kuwapongeza kwa utendaji wenu wa kazi, lakini kubwa na la msingi msiogope kutetea misimamo ya nchi yenu licha ya umaskini wetu” akasema Mwenyekiti wa Kamati.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo inayowajumuisha Mhe.Beatrice Shelukindo,Mhe. Rachel Masishanga, Mhe. Khalifa Khalifa na Mhe. Vita Kawawa. Mhe. Edward Lowassa, licha wa kuwaasa maafia hao kutolegeza buti zao pale linapokuja suala la kusimamia na kutetea maslahi ya taifa na utaifa. Amewapongeza maafisa hao kwa namna wavyofanya kazi kwa uhodari mkubwa ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa hali ya juu wanaouonyesha miongoni mwao.

“ Tukiwa hapa tumejifunza mengi, tumeona mengi, tumefahamu changamoto mnazikabiliana nazo katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku. Lakini pia tumefurahishwa na kuridhishwa sana na mpangilio wa kazi zenu, ushirikiano miongoni mwenu, mshikamano na maelewano ambayo mmejijengea, hili ni jambo jema sana na tunawaomba mliendeleze”. Akasisitiza Mwenyekiti.

Aidha Mhe Lowassa, akasema Kamati yake itakwenda kuzifanya kazi changamoto mbalimbali kwa kushirikiana na wahusika kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi ili kuleta ufanisi zaidi na tija.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti amewahimiza maafisa hao umuhimu wa kujiendeleza kitaaluma na kusisitiza kwamba elimu haina mwisho na hasa katika dunia ya leo ambayo inachangamoto za kila aina.

Kwa upande wake Kaibu Balozi, Dkt. Justin Seruhere akizungumza kwa niaba ya maafisa wenzie ameishukuru kamati hiyo kwa kuutembelea Ubalozi na kuahidi kwamba maafisa watazifanyia kazi changamoto zilizoainishwa na wajumbe wa kamati wakati wa ziara hiyo.

Wakiwa hapa New York ujumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipata fursa ya kusikiliza taarifa za utendaji kazi wa kila Afisa kulingana na majukumu ya Kamati yake, taarifa ya masuala ya utawala na fedha na wakapata pia fursa ya kuhudhuria mikutano na mijadala iliyokuwa ikiendelea katika Umoja wa Mataifa, na wakatembelea na kukagua majengo yanayomilikiwa na serikali na yale ambayo yamekodishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2012

    Bora mmemaliza hii ziara. Next time fanyeni video conference kama mambo yenyewe ni kuja huku na kukutana na watu wa ubalozi wa TZ. Hii itasaidia kupunguza gharama za walipa kodi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2012

    Kila m'bongo anatafuta namna ya kuligegeda taifa ndiyo maana malalamiko kutoka kwa wananchi hayapungui.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2012

    Kila jambo watu wanalaumu tu, sasa nini kifanywe? Ulishaona wapi serikali inafanya ukaguzi kwa video jamani? Mkiendelea kuwa na wasi wasi namna hiyo kwa kila mtu basi nanyi wenyewe mtakosa kujiamini. Hakuna gain bila pain. We have to spend money also when tracking government's expenditure. Jamani tupunguze kulalamika, labda na wivu, tuache watu wafanye kazi. Amini, kila mtu analipenda Taifa letu, na kila kazi inataratibu zake.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2012

    Wewe mwandishi wa pili unahitaji kuwa na positive thinking

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2012

    Vizuri kamati ya Bunge ya NUU (Nje, Usalama na Ulinzi) kutupatia mrejesho (feed-back)juu ya ziara yao.

    Kwa staili hii tunaweza kujua utendaji wa kamati za Bunge, ziara za Mawaziri na viongozi wengi wakuu na kuona kama hela ya walipa kodi imetumika vizuri ( valu-for-money).

    Huu ni mwanzo mzuri lakini mrejesho wa ziara hii ya Kamati ya Bunge ya N.U.U ingeweza kutoa ripoti ya uwazi zaidi ili kuondoa shaka ya umuhimu wa ziara/mafunzo haya.

    Ila ni mwanzo mzuri.
    Mdau
    Mlipa Kodi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2012

    Ukaguzi. Nana kasema hii Kamati ilienda kukagua Bilozi. That's wrong kabisa. Walienda kujifunza mambo mbalimbali huko nje. Ni CAG tu ndo mkaguzi wa fedha zetu. la kujiuliza ni je hizi ziara za waheshimiwa zina tija kwa nchi.... Wametumia sh. Ngapi za walipakodi. Ni kwanini hawaendi Burundi, Rwanda, Ethiopia, misri, UAE, etc.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2012

    Kazi ya ukaguzi wa mali ya serikali inafanywa na mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) na wala siyo wabunge wa kamati. Duplicate work? Kuna haja ya kuainisha priority na kuangalia jinsi gani tunaweza bana matuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...