Baadhi ya wachezaji wa Bongo Fleva wakiwa mazoezini.
Bongo Fleva wakiwa ‘siriaz’ mazoezini.
Kala Pina (katikati), akipasha misuli na wenzake.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Suma G akijinoa.
Amini Mwinyimkuu na wenzake.
JB (wa kwanza kushoto) ‘akijikomaza’.
Vicent Kigosi ‘Ray’ wa Bongo Movie akijiwinda kwa mpambano wa Jumamosi.
Mshambuliaji wa kulia wa ‘Bongo Movie’, Hartman Mbilinyi akipiga shuti wakati wa mazoezi.
Inspector Haroun wa Bongo Fleva akiwa mazoezini.
Mussa Issa ‘Cloud’ wa Bongo Movie (kulia) akiwania mpira na mwenzake.
---
TIMU za mpira wa miguu za wasanii wa muziki, Bongo Fleva, na wacheza sinema, Bongo Movie, jana zilizidi kutoleana vitisho kwenye mazoezi yaliyozikutanisha katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’, alisikika akisema kuwa hakuna mechi itakuwa chungu kwa Bongo Fleva kama ya Tamasha la Matumaini itakayofanyika Jumamosi hii, ambapo wanatarajia kuwapakiza mvua ya magoli.
Nao Bongo Fleva, kupitia mchezaji wao Kala Pina, walisema mazoezi wanayoyapata kutoka kwa kocha wao, Seleman Matola, wanawaomba Bongo Movie wajitoe mapema mechi hiyo kwani moto wake utakuwa mkali isivyo kawaida. (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2012

    hivi siku hizi Kalapina anaimba Bongo fleva.......na sio hip-hop tena? au ndio komesho. naomba nijuzwe wadau

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2012

    Mdau hapo juu,
    Nadhani mada ilikosewa, ilitakiwa itamkwe 'Tamasha la Mpira kati ya Wanamuziki wa Kizazi kipya na Wacheza filamu'. Grouping Bongo Fleva na Hip Hop za akina Kala pina ni makosa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...