Baadhi ya wachezaji wa Bongo Fleva wakiwa mazoezini.
Bongo Fleva wakiwa ‘siriaz’ mazoezini.
Kala Pina (katikati), akipasha misuli na wenzake.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Suma G akijinoa.
Vicent Kigosi ‘Ray’ wa Bongo Movie akijiwinda kwa mpambano wa Jumamosi.
Inspector Haroun wa Bongo Fleva akiwa mazoezini.
---
TIMU za mpira wa miguu za wasanii wa muziki, Bongo Fleva, na wacheza sinema, Bongo Movie, jana zilizidi kutoleana vitisho kwenye mazoezi yaliyozikutanisha katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’, alisikika akisema kuwa hakuna mechi itakuwa chungu kwa Bongo Fleva kama ya Tamasha la Matumaini itakayofanyika Jumamosi hii, ambapo wanatarajia kuwapakiza mvua ya magoli.
Nao Bongo Fleva, kupitia mchezaji wao Kala Pina, walisema mazoezi wanayoyapata kutoka kwa kocha wao, Seleman Matola, wanawaomba Bongo Movie wajitoe mapema mechi hiyo kwani moto wake utakuwa mkali isivyo kawaida. (Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
hivi siku hizi Kalapina anaimba Bongo fleva.......na sio hip-hop tena? au ndio komesho. naomba nijuzwe wadau
ReplyDeleteMdau hapo juu,
ReplyDeleteNadhani mada ilikosewa, ilitakiwa itamkwe 'Tamasha la Mpira kati ya Wanamuziki wa Kizazi kipya na Wacheza filamu'. Grouping Bongo Fleva na Hip Hop za akina Kala pina ni makosa