
Katika dunia ya leo, kuwa na website sio kitu cha kuchagua tena bali ni cha lazima, ila kuwa website inayofanya kazi kwa gharama nafuu ni chaguo madhubuti. Katika kulitambua hili, timu nzima ya AfroIT.com inakuletea mafundisho ya kutengeneza website kwa kutumia award winning open source Joomla bila gharama yoyote. Mafunzo haya yenye module 17 hadi sasa yameshafikia module ya kumi.
Mafunzo haya yanayotolewa kwa kiswahili tena kwa mtindo wenye uhalisia wa Mtanzania, yanawafaa watu wote kuanzia mtengeneza tovuti, mmiliki wa blog nk, hivyo wakati ni huu sasa.
Unaweza kuangalia mafunzo haya kwenye Youtube Channel yetu au moja kwa moja toka kwenye tovuti yetu yaAfroIT.com. Pia unaweza kudownload na kuweka kwenye simu, kompyuta, iPad nk na ukawa unapata mdidi kila ulipo.
Pia usisite kutumia Forums kwa ajili ya majadiliano pindi unapopata utata kwenye mafunzo na kuhitaji msaada.
The Team
Waoh.....we need such creativity in our country ankal! Hongereni sana jamani.mitawasaidia vijana wetu wanaoshinda vijiweni kupata cha kufanya angalau.....congrats big guys!
ReplyDeleteSijapenda hicho kitufe cha juu kabisa katika hiyo image.Muwe makini na shepu mnazozitumia.
ReplyDelete