Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mh Bernardi Membe unahadhi ya Kuwa Raisi wa nchi yeyote Duniani kwa sababu za upeo wa kisiasa ulionao.
    Wanasiasa vijana wanapaswa kujifunza na kuishi kwenye ujuzi ulionao kwa faida ya nchi na viongozi wanaokuja.

    Tunahatua moja tu imebaki ya kuvuka ili kuijengea jamii yetu ya kizazi cha Tanzania ijayo iwe Nchi yenye Mafanikio makubwa na mfano wa kwanza Barani Afrika .
    Ila lazma tofauti za kisiasa na Udini zidhibitiwe mapema.

    Maadui wa vyama watakuwa ndani ya vyama vyenyewe kama hatutaangalia kiundani.

    Tusijenge vyama vya kiuadui na kufanya wananchi wawe waoga na kutojiushisha na utetezi wa haki zao bila kusababisha madhara kwa jamii na kuwafanye watofautiane.

    Pia wabunge wengi wasilaumu Serikali bila ya kuthibitisha malalamiko yao kisayansi.

    Wabunge wanamajukumu ya kuleta maendeleo moja kwa moja kwa jamii iliyowachaguwa kama watatumia mda wao kwenye vitendo vya maendeleo zaidi ya mazungumzo Bungeni.

    Serikali iwe inaorodha ya wazi kwa wabunge waliofanya vizuri kwenye ujezni wa jamii yao, ili wananchi wajuwe tofauti ya propoganda na uongozi wa kweli.

    Nchi nyingi zilizoendelea zimepitia hatua tulio nayo sasa ziwe ni za Ulaya Amerika n.k ,Cha msingi ni kuimarisha utaifa na tuwe na upendo na subira ya kweli bila kupandikiza tofauti.

    Tatizo letu ni kwamba tumetoka kwenye umaskini na sasa tunahatuwa ya kupeana majukumu ya kupangalia utumiaji wa mali zetu kwa Tanzania ijayo yenye mafanikio.

    Mimi ni CCM damu,lakini sikubaliani na kitu chohcote kinacholenga kugandamiza maisha ya Mtanzania, watanzania wengi wa umri wangu tumerith CCM kutoka kwa familia ,lakini tujuwe CCM ya sasa inamajukumu tofauti na ile ya zamani.

    Kuhusu kuwashirikisha watanzania walio nje ya nchi Serikali iangalie kwa undani.
    wako watanzania wanaoshiriki kwenye shughuli za kibalozi na vyama ,na wapo walioamuwa kutoshiriki kabisa.
    kwa Mtanzania yeyote anaeishi au aliyeishi nje ya nchi ataelewa ni kwa nini.

    Namaana ya kwamba hatupo imara kwenye ushirikiano wa kweli tunapokuwa nje ya nchi.

    Tusipofanya hivi tutakuwa tumewanyima haki tena ukizingatia kuwa hawatajielezea,ila watakuwa ni Watanzania milele na wanahaki ya kuja kuishi nyumbani kwa siku zijazo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...