Sasa mwezi mmoja na ushee hatujaona hata tone la maji hapa Tandale kwa AliMaua jijini Dar karibu na Heko Motel, cha kushangaza zaidi vitongoji vilivotuzunguka vinapata maji kama kawa; miaka mitatu iliyopita tulikua tukipata maji mengi sana hata mchana maji yalikua yanatoka, kasheshe ikaanza baada ya mradi wa wachina kupita na hali inazidi kuwa mbaya kadiri siku zinavyo kwenda mbele.
 
Meneja wa Dawasco wa pande hii sijui kama ana taarifa hii ila kuna watu ndani ya ofisi yake wanafahamu na hakuna kinachofanyika; tunaomba msaada kutoka ngazi za juu kwani wananchi wa maeneo haya tunateseka sana. 
 
Mdau Kwa Ali Maua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2012

    Hili eneo ni kweli kabisa kuna tatizo kubwa sana la maji; tatizo ni kwamba hakuna kiongozi yeyote anaye fanya jitihada zozote za kushughulikia tatizo hili, au angalau kuelezea tatizo nini na litakwisha lini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...