Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni Milioni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Aisee mi siku zote nilidhani waziri mkuu wa uingereza anaitwa David Cameroon kumbe ni Donald. Asante kutuelimisha upya michuzi.
ReplyDeleteJamani, huyu jamaa anaitwa David sio Donald. Wenzetu mambo ya majina wanayajali sana. Angalia kaka Michuzi.
ReplyDeleteHuyo anaitwa David William Donald Cameron.
ReplyDeleteAnkali jina la waziri mkuu wingereza sio DONALD ni DAVID CAMERON. Asante. Sasa hii mikutano inatusaidiaje watanzania wa vijijini? Mikataba na makubaliano yanatekelezwaje kwetu wa huku vijijini?
ReplyDeleteHuu ni wakati mzuri wa wakazi wa kusini, kama Mtwara na Lindi kung'ara,maeneo karibu na pale lazima infrastructure pamoja na social services ziwekewe kipaumbele. Na huo mkataba tunaomba tu uwe mzuri kama ndo yale ya 3% ni bora waache.
ReplyDeleteMichuzi waziri mkuu wa uk anaitwa David Cameron sio Donald
ReplyDeleteKumbe £80 tu za UK ni kama Tsh 125 trilioni za kibongo nilikuwa sijui !!!
ReplyDeleteHayo ndio matatizo ya kuchamba kwingi...muende google mkaangalie majina yake, sio mjitie mnajua kusahihisha saaana! Anaitwa David William Donald Cameron.
ReplyDeletejamani jina limekuwa issue kuuuubwa,badala ya kucomenti mambo ya maendeleo-so what kama Michu kateleza,au kwa vile ndo waziri wenu mkuu, common guys get over with and start being real. Zebedayo
ReplyDeleteBadala ya kucoment mambo muhimu mnaangalia jina, sasa kakosea nini?! kama mlikuwa hamlijui hilo la Donald ni juu yenu. Stress zinawasumbua!!!
ReplyDelete