Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Silaa wakati meya huyo alipomtembelea hivi karibuni na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya Manispaa hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Silaa wakati meya huyo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya Manispaa hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Silaa na viongozi wengine kutoka manispaa ya Ilala waliofuatana na Meya huyo Ikulu jijini Dar hivi karibuni.Picha na Freddy Maro,Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2012

    Hilo ndo vazi la Taifa sasa, mnaonaje?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2012

    Jamani mi nampenda huyu mkaka. Huwa anakuwa kama vile anaangalia juu kumbe anaangalia level. Na pua yake ina rangi nzuri, yaani kama maziwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2012

    Vijana si hawa wa CCM, kijana mzuri,, anasura ya rabasamu ukimuangalia katulia na kwa mcho tu unamuona muadilifu. Na ni mwanasiasa, ila mpka waandamane wapende majukwaani ndio mjue kama wapo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2012

    Anonymous no.2 hata kama hatukuoni kwa macho ya nyama tuliyopewa na Mwenyeenzi Mungu, tunakuona kwa macho ya rohoni tabia yako ya kuandika mambo ya utani wakati watu wako serious unaonyesha wazi ulivyo jirekebishe utaishia kuwa hivyo na kizazi chako. Utamlilia nani? Watanzania tubadilike!!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2012

    hicho ndicho ulichokiona macho na pua baaaaaaaaaaaaaaasi,mie nilijuwa utasema unampenda kwa sababu ni mchapa kazi kumbe..............))) that is BONGO

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2012

    Wewe namba 1 umenianzishia siku yangu ya leo vizuri.Nimeamka kwa kucheka...nimecheka sana hadi mke wangu akaja kuangalia kinachonichekesha na yeye akajikuta akicheka.

    David V

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2012

    Maneno mengi acheni lakini, mimi nafurahishwa sana na uongozi wa Raisi Jakaya. Mnaompaka matope muache amejitahidi. Matatizo ya nchi hayapo kwa viongozi tu yapo kwa watendaji. Hata Nyerere alikuwa na ndoto nzuri sana za kuikomboa nchi hii lakini alikwamishwa na watendaji wake. Tujisafishe kwanza ndo tumshambulie JK.

    Mdau, ughaibuni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2012

    Watendaji wanajirekebisha kidogo kidogo, unafanya mchezo mpaka mkuu wa wilaya ya handeni anapiga kambi msituni ili kupambana na waharibifu wa misitu. Mwakyembe anavyowakosesha raha wenye mabasi ya mikoani...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2012

    NA MIMI NITA SHONA YANGU.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2012

    heehehhe namwona foty kijana kwa nyumaa pale safi sanaaa najua mambo yake safi sasa hv kijanaaa mkazane tu kusoma ikulu kutakuwa kama nyumbni na nyie

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 12, 2012

    Kumbe gwanda limekuwa vazi la taifa.Naona viongozi kibao siku hizi wanavaa gwanda ingawa wao hupenda sana la rangi ya blue kuliko Kaki.

    Peopleeeeesssss..

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2012

    Jerry Slaa una maono sana kijana wewe mimi napenda uchapa kazi wako na nakuombea Mungu akuweke ufanye mengi na wananchi wako waone. JK Mungu akulinde kila siku nakuombea.Viongozi wa Ilala mlio katika picha hii, fanyeni kazi kwa bidii,

    ReplyDelete
  13. Hakuna hata mchangiaji hata mmoja ambae ametoa wazi au mchango wa maana! wote hovyoooooooooo!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 13, 2012

    Katika nchi ya Tz viongozi waadilifu na wachapa kazi ni wachache sana. Umetoa mfano Mwakyembe na huyo DC, Sawa sikatai. Ila kundi kubwa la hao watendaji wana uroho wa maslahi tu hawana nia na maendeleo ya nchi na watu wake.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 13, 2012

    Tanzaniania hasifiwi mchapa kazi...tena huyo ndio huchukiwa kabisa......Mabosi wengine huona mchapa kazi kama anawazibia riziki, hufanya mipango kumuondoa mapema.

    Tanzania ya leo si ya jana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...