Kikosi cha Yanga
 Kikosi cha APR ya Rwanda
 Beki wa Timu ya APR,Mbuyu Twite akimzuia Mshambuliaji machachari wa timu ya Yanga,Said Bahanuz ili asiuchukue mpira kwenye mchezo unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Yanga imeitungua APR bao 2-0.
 Mashabiki wa timu ta Yanga wakiishangilia timu yao baada ya kupata ushindi dhidi ya timu ya APR ya Rwanda katika mchezo uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar ikiwa ni muendelezo wa Mashindano ya Kombe la Cecafa Kagame. 
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na Said Bahanuz dakika ya 28 ya mchezo kipindi cha kwanza,huku mwamuzi wa mchezo huo akiwataka kurudi uwanjani.
 Nizar Khalfan wa Yanga akiwachambua mabeki wa APR.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2012

    Yanga mwendo mdundo .Nadhani kombe watalitwaa tena mara ya pili mfululizo.Mwendo huo huo yanga ,daima mbele ,nyuma mwiko.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2012

    Hivi huyu Bahanuzi amesajiliwa kutokea timu gani? Machachari sana huyu, anatutia hofu sana sisi wengine.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJuly 20, 2012

      Anakutia hofu wewe na nani?

      Delete
  3. AnonymousJuly 21, 2012

    na bado...hzo rasharasha tu! mmezidi sana kelele nyie wenzetu!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2012

    Yanga pawe dozi haooooooooooooooooooooo.
    Yaani raha kweli kweli kweli

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2012

    Ingawa apr walicheza mpira mzuri lakini yanga nafasi walizopata walizitumia vizuri .mabeki walitulia sana viungo makini washambuliaji ndio usiseme hongera yanga kazeni buti mtupe raha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...