WATANZANIA WENZANGU KUNATAARIFA IMTUFIKIA KUNA MTANZANIA ANAEITWA CLARISE NIYOKURU AMELAZWA WASHINGTON HOSPITAL ICU CHUMBA # 2H22 TUNAOMBA UKIPATA NAFASI MTEMBELEE NA KAMA KUNA NDUGU YAKE ANAWEZA KUMPIGIA MARIAM ARAGA (MKE WA DAVID TARABA) SIMU YAKE NI +1 703 963 3546 YEYE NDIYE AMETULETEA TAARIFA HIZI NA HOSIPITALI WANAWATAFUTA FAMILIA YAKE.

CLARISE NIYOKURU ALIANGUKA GHAFLA AKIWA KAZINI NA KUKIMBIZWA ADVENTIST HOSPITAL NA WAO KUMUAMISHIA WASHINGTON HOSPITAL.

TAFADHALI UKIPATA NAFASI MTEMBELEE MGONJWA ANAHITAJI UPENDO WAKO NA KWA KUFANYA HIVYO NI KUONYESHA MAPENZI KWA NCHI YAKO NA WATANZANIA WOTE SOTE NI NDUGU, 
ASANTE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    Ugua pole mgonjwa. Lakini mtoa taarifa, sasa tunaitwa kumuona mgonjwa au kufanya siasa? mbona unalalamika na kulaumu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Asante kwa taarifa, Ila ujumbe kama huu ni vizuri kuwa na address kamili maana unaweza kukuta Washington hospital jina limejirudia mahali pengine na si kila mtu atakuwa anajua Washington hospilal ilipo. Asante kwa kuelewa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2012

    Sawa Ahsante kwa taarifa,

    Pia muelewe kuwa na Pasipoti ya Tanzania sio kigezo kuwa nduguze wapo Tanzania au watakuwa wa-Tanzania, mtu anaweza kumiliki Pasi halali ya TZ kama sehemu ya kuhangaika na maisha wakati yeye akiwa ni mtu wa Kigali-Rwanda.

    Kwa dalili ya jina hilo ''CLARISE NIYOKURU'' pana uwezekano taarifa zifike Ubalozi wa nchi Jirani niliyoitaja hapo JAMHURI YA RWANDA!

    ReplyDelete
  4. Charles Lema, East MongoliaJuly 25, 2012

    Mungu wetu wa Mbinguni amsaidie mgonjwa apone haraka na kutoka Hospital akendelee na kazi zake katika kulijenga taifa.... Hongereni sana watanzania wa D.C kwa kua na moyo wa Upendo namna hii.. hata Uncle pia asante sana unatujali sana sisi Watanzania tunaoishi nje kwa kutoa msaada wa taarifa haraka sanaa pale unapo hitajika.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2012

    DAA POLE NA WENGINE NAWAONEA HURUMA MKIRUDI NYUMBANI MRUDI NA WHEELCHAIR ZENU KABISA MAANA HUKU NYUMBANI HATUTAWEZA KUWABEBA NA MAUMIVU YENU YA MIGONGO.

    ReplyDelete
  6. Majina siku hizi hayafuati nchi wala kabila,mheshimiwa hapo juu umepotoka, je ? wanaoitwa Washington Walles hao tuwapeleke nje gani ?? Shinyanga na Mwanza yako majina kama haya na mwalimu wangu darasa la saba alikuwa anaitwa jina hilo. Wewe wahi wodini kaangalie mgonjwa,mambo ya kujilipua waachia uhamiaji. Zebedayo Msema kweli

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2012

    Muwe na jumuiya ya tanzania huko na mwenyekeiti wenu halafu kitu kama hii mnaanza kuatafutana, just that simple

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2012

    ASANTE SANA KWA TAARIFA PIA POLE SANA MGONJWA TUNAKUOMBEA MUNGU UPONE HARAKA, KWA WATANZANIA MLIOKO NCHI ZA NJE NATUMAINI KUWA MNAZO JUMUIYA ZENU AMBAZO UMUHIMU WAKE NDIO KATIKA KIPINDI KAMA HIKI CHA MARADHI HATA IKITOKEA MTANZANIA KUFARIKI, KWAHIYO JITAHIDINI KUJIANDIKISHA NA KUTOKA ANUWAN NA NAMBARI ZA SIMU ZA WAZAZI NDUGU HATA JAMAA ZENU WALIOKO WALIOKO HUKU ILI KUONDOA USUMBUFU WAKATI TATIZO LINAPOKUTOKEA.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2012

    Zebedayo Msema ukweli,

    Hapo jamaa Mtoa Maoni wa juu amegusia uwezekano jamaa anaweza kuwa Raia wa Tanzania na akawa na ndugu hukooo Rwanda!

    Hapa sio suala la kuhoji Uraia bali uwezekano wa ndugu huko.

    Angalia pana tofauti Kati ya Christian-French names, hadi Christian-Portuguese names , hadi Christian-English names,

    1.Dalili ya kwanza.
    Ni nadra sana ukakuta mtu Mtanzania anaitwa hiyo French name Clarise, au Antoine, Francois.... kama unavyojua hatukutawaliwa na Mfaransa bali Rwanda,Burundi na Congo huko.

    2.Dalili ya pili.
    Hiyo jina la mwisho NIYOKURU pana uwezekano mkubwa wa 'Ubanyamulenge' hapo,,,kwa kuwa jamii ya Makabila ya ki-Tanzania majina ni ya akina Maganga,Mkude,Mhando na watani wako akina Shirima, Minja na Mushi !

    Upo hapo?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2012

    CLARISE NIYOKURU:

    Huyo pana dalili kubwa akwa ni Banyamulenge wa Burundi au Rwanda, kwa kuwa Tanzania ni mara chache watu kuwa na majina ya kwanza yanayoashiria Kifaransa(Clarise) na jina la mwisho Makabila yetu majina yanajulikana hiyo (Niyokuru) sio ktk Makabila ya Ki Tanzania.

    Sema jamaa anaweza kuwa Raia halali au anaweza kuwa ni Mchakarikaji kama ndugu zetu wengi waBongo ametumia tu Kitabu chetu kifikia lengo lake la safari Majuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...