Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala ya Sheria wa Kampuni ya Bia (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange (kushoto) hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika tarehe 5 Agosti mwaka huu. Wanaoshuhudia ni George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wadhamini wakuu wa klabu hiyo na Katibu wa Simba, Evodius Mtawala. (Picha: Executive Solutions).

Ikiwa ni sehemu ya udhamini wake kwa klabu ya Simba, bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu hiyo kwa ajili ya mkutano mkuu utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi hundi hiyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema: “Kilimanjaro Premium Lager inatambua wajibu wake na ina nia ya dhati kuendeleza soka nchini. Kwa kwa kuzingatia hilo tungependa kuona maendeleo ya Simba na ndio maana tunaiunga mkono klabu hii katika mkutano wake mkuu. 

Tunaamini kuwa mkutano huu utaimarisha uhusiano uliopo kati ya klabu na wanachama wake kwa kuwapa fursa ya kuhakiki mwelekeo wa klabu yao waipendayo.Kavishe alieleza zaidi, “Mtu anapoangalia historia ya klabu hii kongwe ambayo imejengeka kutokana na rekodi nzuri ya mafanikio kwa muda mrefu utaona kwamba ina mamilioni ya wapenzi nchini. 

Soka ndio ndio mchezo mkubwa zaidi hapa Tanzania na bia ya Kilimanjaro imekuwa ikitoa mchango mkubwa kusaidia mchezo huu na ndio maana leo tunasaidia mkutano mkuu wa Simba ili kusaidia kudumisha uwajibikaji wa klabu kwa wanachama wake.

“Tunatambua wajibu wetu kama wadhamini wakuu wa Yanga katika kutekeleza mkataba wetu, tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha tunalipeleka soka la Tanzania kwenye kilele cha mafanikio”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...