Benki ya NMB jana imekabidhi zawadi za tani za saruji
na mabati kwa washindi wa droo ya kwanza
ya promosheni ya ‘Jenga maisha yako na NMB’ iliyofanyika terehe 11 Julai
2012.
Wateja
wa Benki ya NMB, Victoria Maliseli, Ramadhan Mguya,Rehema Mohamed,Rose Mandera
na Richard Makara wakifurahia kupata zawadi ya mabati 50 kila mmoja na tani ya saruji kila mmoja(mabati wawili
kushoto na tani ya saruji watatu kulia) pamoja na Mkuu wa idara yaMasoko na
mawasiliano wa NMB Imani Kajula
Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika
katika tawi la NMB Airport, Mkuu wa idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani
Kajula alisema kwamba, “NMB sasa inawezesha ndoto za watu kuwa kwelileo
tunakabidhi tani za saruji na mabati.Hatimae ndoto za washindi sasa zimekuwa
kweli na tunaamini promosheni hii sio tu kwamba itaongeza tabia ya kujiwekea
akiba lakini itasaidia wateja walioshinda kufikia malengo waliojiwekea na pia
kuboresha maisha yao”.
Mteja wa NMB Bi. Victoria Marisel akipokea mfano wa hundi yenye
thamaniya mabati 50 kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja wa NMB tawi la NMB Airport,
Deogratius Mahawe.
NMB kwa kutambua kuwa watanzania wengi wanaweka
akiba ili kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea yakiwa ni kujenga nyumba,kusomesha watoto na kufikia malengo mengine muhimu maishani mwao, ilizindua promosheni inayowezesha wateja wa
NMB Bonus Account an NMB Junior Account kuingia kwenye droo ya kushinda tani ya
saruji,mabati ya kuwezeka,amana maradufu,ada za shule,fulana za NMB pamoja na
mabegi ya shule kupitia promosheni ya Jenga maisha yako na NMB.
Katika droo ya kwanza washindi zaidi ya 167 walijishindia
zawadi mbalimbali. Kushinda ni rahisi
sana, fungua akaunti au ongeza amana kwenye NMB Bonus Account au
NMB Junior Account upatea riba ya kuvutia ambayo inaweza kuwa hadi asilimia 10 kutegemeana na kiwango cha
amana ilichoweka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...