MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipokea msaada wa fedha taslim shilingi milioni 10 kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Taifa (NSSF), Juma Kintu ikiwa ni msaada kwa waathirika wa ajali ya meli ya Mv.Skagit iliyotokea juzi. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Balozi seif zilizopo katika Baraza la Wawakilishi Mbweni Wilaya ya Magharibi.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipokea msaada wa fedha taslim shilingi milioni 10 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Khamis Fil fil ikiwa ni msaada kwa waathirika wa ajali ya meli ya Mv.Skagit iliyotokea juzi Makabidhiano hayo yalifanyika ofisini kwa Balozi seif zilizopo katika Baraza la Wawakilishi Mbweni Wilaya ya Magharibi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewanasihi Wananchi kuendelea kuiamini Serikali katika kupokea Taarifa zake hasa wakati wa kutokea Majanga na Maafa.
Nasaha hizo amezito hapo katika Ofisini yake iliyopo Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akipokea mkono wa Pole kutoka kwa Taasisi mbali mbali za Umma na Kijamii.
Salamu hizo za mkono wa pole zimetolewa kwa Balozi Seif na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } na ule wa Hifadhi ya Taifa ya Jamii ya Tanzania { NSSF } ambapo kila moja ilikabidhi mchango wa Shilingi Milioni 10.
Balozi Seif alisema Jamii kujenga tabia ya kuiamini Serikali hupelekea kuwepuka kuchanganywa wakati wa kupokea Taarifa hizo kutoka vyombo vya Habari vinavyopokea Baadhi ya Taarifa zisizo rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa mifuko hiyo ya Hifadhi ya Jamii Bara na Zanzibar kwa kufikiria jambo hilo muhimu la kutoa mchango ambalo Taifa linahitaji kuungwa mkono katika kukabiliana nalo.
Aliuhakikishia Uongozi wa Taasisi hizo kwamba michango hiyo itasimamiwa vyema kwa ajili ya kuwafika waliohusika kwa kutumia utaratibu uliotumika wakati wa ajali iliyotokea Mwaka jana.
Alisema licha ya zoezi la uokozi kuwa na gharama kubwa lakini Serikali inaendelea kutoa huduma zote za mazishi na usafirishaji wa maiti zinazopelekwa Tanzania Bara ambazo zilipatikana kutokana na ajali ya Meli ya M.V Skagit hapo juzi.
Aliongeza kuwa shughuli hiyo ikiwemo gharama za vyombo, mafuta, Chakula na uokozi zinahitaji kuungwa mkono na taasisi na jumuiya ya kiraia ndani na nje ya Nchi. “ Serikali imeshachukua jukumu la kuzizika zile Maiti zilizoshindwa kutambulika hadi sasa, kuzisafirisha maiti tatu hadi Tanzania Bara pamoja na familia nne wakati maiti moja ya raia wa kigeni bado haijatambulika”. Alifafanua Balozi Seif.
Alisisitiza kwamba katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo wazamiaji wa Israel walioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wameamua kusaidia kazi ya uokozi kwenya Meli hiyo ili kuendelea kutafuta miili ya Watu iliyopotea.
Mapema Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Ndugu Khamis Phil Phil Than alisema yapo mambo mengi kwenye tukio hilo la Maafa ambayo yanahitajika kupata msukumo kutoka kwa Washirika, Taasisi na Jumuiya za Kiraia. Ndugu Phil Phil alisema mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar umekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake yaliyolenga zaidi kwenye eneo la Jamii.
Naye kwa upande wake Ofisa Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania { NSSF } kutoka Makao Makuu Mjini Dar es salaam Nd. Juma Kimtu alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo imeamua kutoa mchango huo baada ya kuona uzito Maafa yaliyotokea ambayo yameigusa Jamii yote.
Ndugu Kimtu alisema Serikali kwa kuwa ni ya watu haina budi wakati wote kusaidiwa hasa katika masuala ya Majanga na Maafa ambayo kwa kiasi kikubwa huigusa Jamii yote.
Na
Othman Hamisi Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar
Wanastahiki pongezi na Munyaazi Mungu awaongezee.
ReplyDeleteSwali langu ni dogo tu, jamani hata taasisi kubwa kama hizi bado zinaenda kwa mtindo wa 47 wa mapesa taslimu hata kwa kiasi kikubwa kama hicho???
Tatizo sio hilo wakitumia njia ya acc itakuwa wao hawaonekani na yale mapesa mtu itakuwa picha hazipigiki
ReplyDeletekwani wengi wao hawa wanaotowa mapesa wanataka waonekane ndugu yangu
kwa kweli nimeshangaa. kwenye nchi za wenzetu suala la michango kama hii hutolewa dokezo "DO NOT BRING CASH."
ReplyDeletePOLENI SANA! LAKI NI VEMA KUTUMIA HUNDI KULIKO KUONYESHA VIVYO VITITA VYA MAPESA!
ReplyDelete