Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan naomba niwajulishe kwamba tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT,iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha wenzetu wengi kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Tunawapongeza na kuwashukuru taasisi mbali-mbali na watu binafsi wanaofanya kazi kubwa kukabili zoezi la uokoaji, na wale waliotufikishia habari hizi. Tunawashukuru wale wote waliopata taarifa na kuelekea kwenye eneo la tukio na kuanza uokoaji mara moja.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania, na Watanzania wote tunaoishi nchini Japan, tuko pamoja nanyi,na pia tunaungana na Watanzania wenzetu wote kutoa pole kwa wafiwa, na kuwaombea majeruhi waweze kupona kwa haraka. 

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote nakuwapa nguvu na uvumulivu ndugu na jamaa, katika kipindi hiki kigumu.

NJENGA, Rashid
Mwenyekiti,
Jumuiya ya Watanzania Waishio nchini Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2012

    Tumewapata,tuko pamoja.Blog ya jamii kuna 'ngoma' iko ziwa 'Magharibi' inaitwa M.V Victoria inafanya safari zake kati ya Mwz-Bukoba.Ni meli muhimu sana kwa uchumi wa mikoa hii,kinachotakiwa ni ukaguzi wa hali ya juu manake imekula chumvi kweli kweli.Sasa hivi kuna lami MWZ-BK,hii meli siyo ya kung'ang'ania sana isije kutuletea balaa siku moja.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...