Kwa niaba ya watu wa Marekani tunapenda kutoa rambirambi zetu za dhati kwa watu wa Tanzania na wale wote walioguswa na ajali ya Meli ya MV Skagit iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam, kwenda Unguja, Zanzibar tarehe 18 Julai 2012.
Marekani imeguswa na inaahidi kuwasaidia watu wa Tanzania katika kukabiliana na janga hili. Tayari tumeshatoa masaada wa madawa na vifaa tiba vinavyohitajika wakati wa dharura pamoja na wahudumu wa afya ili kusaidia mamlaka za Zanzibar kukabiliana na janga hili.
Tumetiwa moyo sana na hatua za uokozi na kuwahudumia waathirika wa ajali hii zinazochukuliwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar.
Tunatoa wito kwa mamlaka za Tanzania kuweka mipango thabiti ya kukabiliana na kushughulikia majanga (disaster management planning efforts) ili kuzuia tukio kama hili lisitokee tena katika siku zijazo.
Alfonso E. Lenhardt
Balozi wa Marekani - Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...