Jumuiya ya watanzania waishio Kansas City (TAKC) na vitongoji vyake imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya Meli ya MV. Skagit iliyotokea wiki hii karibu na kisiwa cha Chumbe.
Tunaungana na watanzania wote kawapa pole ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao na vile vile tunawatakia kila la heri majeruhi wote wapate kupona haraka na kurudi kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
Imetolewa na:-
John Adhero – Raisi wa Jumuiya ya Watanzania Kansas City (TAKC).
email: kamati_takc@hotmail.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...