Na Said Powa,Globu ya Jamii - Dar es Salaam

ZOEZI la kukata umeme na kukamata wezi wa umeme kanda ya Tanesco Temeke Liliendelea jana ambapo watu wanne wameshikiliwana na Jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme kwa mfumo wa kuchezea mita.

Akizngumza kwenye operesheni hiyo Meneja wa kanda hiyo Richarld Mallamia, ambaye ndiye aneongoza zoezi hilo la nyumba hadi nyumba alisema, zoezi hilo ni endelevu kutokana na watu kujenga mazoea ya kuiba umeme kwa kuwatafuta vishoka ambao uharibu mita ili zisisome na kuiba umeme.

Kwenye zoezi hilo ambalo jana lilifanyika eneo la Mbagala Rangi tatu nyumba moja ilikutwa tangu imeunganishwa umeme wa luku kwa zaidi ya miaka 10 lakini umeme waliotumia kwa kipindi chote hicho haujafika unit 1000 kiwango ambacho watu wakawaida hutumia kwa mwezi mmoja tu.

Akifafanua hali hiyo kitaalamu Mkaguzi wa umeme wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani Elia Shimwela, alisema kiwango kinachoibwa kwenye nyumba hiyo ni kikubwa hasa ukizingatia kuna vifaa vingi vinavyotumia umeme.

“Hawa wananunua umeme kama geresha tu ili mfumo wa Tanesco uonekane kama ni wananunua umeme kwa kiwango cha chini lakini kimsingi umeme wanaotumia wote wanaiba tu, kwahiyo wateja wanamna hii tunawachukua na kuwafungulia mashtaka ya wizi mahakamani,” Alisema Shimwela.

Hadi jana wateja wote ambao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani wamefikia 17 ambapo imeelezwa muda wowote zitakapokamilika taratibu za mashtaka watapandishwa kizimbani.

Katika hatua nyingine mmoja wamiliki wa Jengo la Ghorofa mbagala Rangi tatu nyumba yake imekutwa imeunganishwa umeme kwa mfumo wa wizi huku akiwa na vifaa vingi vinavyotumia umeme hali iliyowastua wakaguzi hao na kusababisha kumchukua aliyechiwa kusimamia jengo hilo hadi atakapo kwenda mwenyewe kwenye kituo cha Polisi Kilwa Road.

Wizi wa umeme kwenye kanda hiyo umekua ukisababisha hasara ya Tsh89 Millioni ila mwezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Hii haina maana kwa Tanesco kukamata vijizi vidogo-vidogo vya umee. Cha kwanza na cha msingi waangalie ni kwa nini watu wanaiba umeme ambao wizi huo ni asilimia ndogo sana ya matumizi mabaya ya Tanesco yanayochangia bei za ajabu za umeme. Jaribuni kukomesha uzembe wa utendaji kuliko kuhangaikia vitu ambavyo havina maana. Mkizingatia hilo huo wizi hautakuwepo,

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Hiki ndo ki mfumo cha taifa letu ukisikia nchi mifumo yake ni butu ndo kama hivyo nawashangaa tanesco kwani inabidi wakashangae uzembe wao na si wezi.nchi yote iko hivo ukisikia mifumo isiyofanya kazi ndo kama hiyo.bado sekta zote zijichunguze.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2012

    Tanesco waboreshe utendaji wao wa kazi pamoja na kutoa huduma bora waone kama wizi hautapungua. Watu wanaiba kwa sababu ya kuzungushwa zungushwa wanapotaka huduma. Tanesco toa kwanza boriti ndani ya jicho lako kabla huja toa kibanzi ndani ya jicho la mwenzio!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2012

    Jamani TANESCO, mtu akinunua umeme wa Sh. 10,000 anapata unit za thamani ya karibu Sh. 6,000/- tu. Fedha zilizosalia hugawiwa kwa percent kwa taasisi kama EWURA, REA, TRA (kodi), n.k. Hivi kweli mlala hoi kuchangia taasisi kama EWURA ambao wanaishi maisha ya anasa pale Samora Avenua na wameshindwa hata kutumia hizo fedha wanazo pata kufungua Ofisi mikoani ili kutatua matatizo ya wananchi kibao, ni sahihi jamani??? Hao REA (Rural Energy Agency), kwa nini wasitafute vyanzo vingine mpaka wasubirie hela ya mlala hoi??? Kwa nini wasiwe wabunifu kama agency nyingine? Kama Serikali haikuwa tayari kuanzisha agency kama hiyo kwa nini waliharakisha na kuja kuwaumiza wananchi? TANESCO wizi huo utachukua muda kuisha, kwani kwanza nchi hii ni kubwa sana lakini pia sababu kama hizo hapo juu zinachangia watu kuiba umeme.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2012

    Kule Mikocheni hamkufika bado. Wafanyakazi wenyewe wa TANESCO ndio wanaounga umeme huo. Kuna mtu umeme unatokea kwenda mabanda ya uwani. Barabarani hana hata mti wa umeme.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2012

    Ni ajabu na kweli!

    Jambo la ajabu hili!

    Maafisa waandamizi Tanesco wanatuhumiwa kwa wizi wa Tshs. 296 BILIONI leo hao hao wanawakamata wezi wa wizi wa (Tsh.30,000/=) Elfu Thelathini?

    Hi si ndi operesheni ya kutukanda mafuta kwa mgongo wa chupa?

    Au funika kombe mwanaharamu apite?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...