Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi –Zanzibar

Zoezi la kuitafuta Meli ya MV Skagit linalofanywa na Wazamiaji wa Majeshi na Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, limezidi kuwa gumu baada ya wataalamu hao kushindwa kuiona meli hata baada ya kuzamia na kuisaka meli hiyo katika eneo ilipozama meli hiyo.

Meli hiyo ambayo ilipinduka na kuzama katika eneo la kisiwa cha Chumbe umbali wa 14 Notcomail vipimo vya majini, haijaonekana tena tangu siku ya tukio.

Wakizungumza baada ya kusitisha zoezi hilo, Wazamiaji hao wamesema wamelazimika kuzamia chini ya bahari na kufanya uchunguzi katika eneo la upana wa zaidi ya kilometa moja bila ya kuiona meli hiyo.

Washiriki wa zoezi hilo kutoka Jeshi la wananchi, Polisi,KMKM, Mamlaka ya Bandari Zanzibar pamoja na makampuni ya watu binafsi katika utafutaji wa meli hiyo kurudi mikono mitupu kwa sababu ya uhaba wa vifaa.

Wakizungumza katika eneo tukio baadhi ya wazamiaji hao wamesema kuna uwezekano kuwa meli hiyo imekokotwa na maji katika kina hicho cha bahari.

Wamesema kuwa ili zoezi hilo lifanikiwe ni lazima vipatikane vifaa maalumu vitakavyosaidia kuchunguza mali ilipo meli hiyo kabla ya wazamiaji hawajafikaa katika eneo hilo.

“Meli hiyo imeshindikana kuonekana kutokana na ukosefu wa vifaa vya kusaidia ugunduzi wa mahali ilipo meli hiyo”.

Alisema Bw. Ali Ramadhani, kutoka Kampuni ya Easy Blue Divers. Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni Fish Finder na Eco Sounder pamoja na Soner Ditector.

Naye Bw. Issa Juma Mohammed, wa Kampuni ya Azam Marine, amesema kuwa wao wana uwezo wa kuzamia kina cha urefu wa mita zaidi ya 50 chini ya bahari na vikiwemo vifaa hivyo vitawawezesha kubaini eneo ilipo meli hiyo kabla ya wao kuanza uzamiaji.

Zoezi la kuitafuta meli hiyo lilianza jana (juzi) kwa lengo la kutafuta miili zaidi ya watu waliozama pamoja na meli hiyo baada ya maili zilizokuwa zikiielea kutoonekana tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Sasa hao wazamiaji kama wameweza kuzamia chini ya bahari na kuchunguza katika eneo la UPANA wa zaidi ya 1km bila mafanikio yeyote. Je, in 'depth' (kwa kina kwenda chini) wamefika umbali kiasi gani? Mana wameelezea mapana tu na marefu how long wamezamia. Si ajabu hawakwenda deep tosha, mbali ya huo ukosekanaji wa hivyo vifaa husika vilivyotajwa hapo, hali iliyopelekea kutopata alau fununu yeyote ile ya kuweza ku-locate Boat hiyo ilipojikita au kuwepo.

    Tatizo hadi leo hii, usafiri wetu wa baharini hauna taratibu zozote zile au za kutosha, kufuatia suala zima la 'healthy and safety' kwa abiria wake. Tunakuja kutaamaki too late, ndio tunaanza kupiga kele na kutowa lawama huku na kule, wakati umma usio na hatia yeyote umeshateketea. Ilikuwa funzo tosha kufuatia ile ajali ya M.V.SPICE iliyotokea on the 10th September, last year. Lakini bado hakuonekani umakini wowote uliokuwa umechukuliwa au tahadhari zozote, japokuwa ajali haina king, lakini tahadhari kabla ya hatari ni bora zaidi. MWENYEEZ MUNGU WAREHEMU, UWAGHUFIRIE KWA YOTE NA UWALAZE PEMA PEPONI WAJA WAKO WOTE WALIOANGAMIA KATIKA ZAHMA HII NA UWAPE TAKHFIF WAPONE SALAMA WOTE WALIONUSURIKA - AMEN.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    inna lilahi waina illahim rajiun cha muhimu na chamsingi kuowambe marehemu wetu dua na tukiomba dua tunapigwa mabomu na kumwagiwa maji sijui nisemeje.

    rahman awalaze pema peponi amin pamoja na sisi tusioijua siku yetu tupo njiani kuwafuata.

    rahma awape tahfif na ustahamilivu wafiwa wote na ramadhan kareem/mubarak.

    kuna siku kitajulikana chanzo chote hiki kwa sababu damu ya mtu haindi bure rahman kisha sema haya

    wazanzibar na wabara wapenda amani na kuwatakia kheri wazanzibari tujifunze kuogelea kama hatujui ili tujiokowe wenyewe because serikali hawezi kutuokoa sisi hata siku mmoja na wala katika uchunguzi wao hawa kuenda mbali wame ogelea juu juu tu na kuacha maiti na watu walio hai wamekufa wenyewe bila kuokolewa huko chini ya bahari..

    ndo ilivyo hawaku kuogolea mbali wala nini muungano utakufa tu kuna siu mtaki msitake

    ReplyDelete
  3. muungano na ufe,hakuna anayeuhitaji. kama nyinyi wazanzibara mmegundua kuhujumiwa bora mjiondokee,sisi wabara acha tuendelee kukomaa na rais wetu kikwete chaguo la watu.sie si emu oyeeeeee!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2012

    Media zimeandika sana habari za ajali ya Meli hii lakini hatujasikia walipo MABAHARIA(Hasa Nahodha)..Wako wapi wapi hawa??..Wamo kwenda kundi lililonasa kwenye Meli?,Wapo kwenye kundi la maiti zilizoopolewa?,wako kwenye waliokolewa wakiwa hai?.Wametoroka?/wamefichwa kwa sababu za kiusalama?WAKO WAPI??

    David V

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2012

    sure mdau...!hata mimi nilikua najiuliza maswali hayohayo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 24, 2012

    Nyumba yenye nyufa nyingi iko siku itabomoka tu. Muungano wenye faida kwa pande zote ungekuwa na malalamiko machache. Huu wa kwetu malalamiko yanazidi kila jua linapochomoza na chuki inajengeka katika jamii.


    hatutakia MUUNGANO HATUTAKI MUUNGANO NA MTUMALIZE LAKINI MTAMALIZIKA WENYEWE HIVI SASA BECAUSE HATUTAKI MUUNGANO NA DAR MSIZANI NI MALI YENU MTAJUTA MKIJAJUA UKWELI WA MAMBO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...