Naibu Balozi wa Tanzania, London, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga (pili kushoto), akiwapokea rasmi Wanamichezo wa Tanzania, watakao wakilisha Taifa katika Michezo ya Olimpiki leo kabla ya kufanya mazungumzo mafupi na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, katika Hotel ya Churchill, jijini London, Uingereza.
 Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (mbele Kulia), Mkuu wa Msafara, Bwana Hassan Jarufu (mbele kushoto), wakifanya mazungumzo na Wanamichezo wa Tanzania katika Michezo ya Olimpiki, itakayofanyia nchini Uingereza mwaka huu 2012.

Timu ya Tanzania itakayoiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki, itakayofanyika nchini Uingereza, leo wamepata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo mafupi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Hotel ya Churchill, mjini London, Uingereza. 

Mheshimiwa Rais Kikwete, aliwapa Baraka za Watanzania na kuwaomba wajitahidi na kuliwakilisha vyema Taifa na kurudisha jina la Tanzania katika ramani ya michezo kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Wanamichezo hao ambao wataliwakilisha Taifa, wameweka kambi yao katika Chuo Kikuu cha Bradford (Bradford University), katika mji wa Bradford, kabla ya kuhamia rasmi kwenye kijiji cha michezo hiyo (Olympic Village) tarehe 24 July, tayari kabisa kwa kuanza ushiriki wao katika mashindao hayo ya Olimpiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2012

    Wanamichezo ya Olympiki wa Timu ya Tanzania,

    Fanyeni juu chini msimwadhiri Mhe. Raisi wetu JK kama mnavyoona michezo hiyo kwa bahati mbaya au nzuri inajiri huku Raisi akiwa huko ziarani Uingereza.

    Tusije kukosa hada Medali angalau moja au tupate zaidi!.

    Sasa chonde chonde mfanye chochote ili kutukingia aibu kubwa kwa Raisi wetu na kwa ujumla wa-Tanzania wote!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2012

    Tizama wenzetu Meza ilivyoyakawaida kama Meza za Motel au za Mwananyamala za asubuhi kuuzia chai na maandazi, zaidi ya hapo nawaombea Wa-Tanzania wenzangu waliohuko UK wafanye Vizuri katika hayo Mashindano na hongera Raisi kuweza kuwapa moyo vijana wenzetu. MZ

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2012

    Huyo Jarufu ni yule anaefanya kazi BOT? Du! Timu imepata kiongozi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2012

    kila mmoja hapo ana lake rohoni wengine wameshafikiria kujiwasha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2012

    Wewe mdau umeona meza kitu kikubwa wewe mkulima wa wapi??????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2012

    Mbona hujaweka majina na michezo wanayotuwakilisha? Au nusu yao ni officials, maana naona vitambi tu hapo...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2012

    what a shame Tanzania representative hata hawajai kwenye kiganja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...