Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Peter Serukamba akipokea i-pad aina ya Samsung Galaxy kutoka kwa Meneja wateja wa mikataba wa Vodacom Tanzania Bi.Melinda Siara Kamukara Bungeni Mjini Dodoma. Mh. Serukamba ni miongoni mwa Wabunge wanaotumia na kufurahia huduma za mawasiliano za Vodacom chini ya utaratibu wa malipo ya baada.
Ofisa huduma za kiufundi kwa wateja wa mikataba wa Vodacom Bw. Dia Misana akiwaelekeza waheshimiwa Wabunge Raya Khamis (Viti Maalum - Chadema) na Francis Mkosamali (Kibondo - NCCR-Mageuzi) mwenye shati jeupe ambao ni wateja wa malipo ya baada wa Vodacom Tanzania namna ya kujiunga na kufaidi huduma bora za Intaneti za Blackberry (BIS) kupitia mtandao wa Vodacom katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Kutoka kulia Meneja wa Mahusiano ya nje wa Vodacom Tanzania Bw.Salum Mwalim, Melinda Siara Kamukara na Dia Misana wa kampuni ya Vodacom wakiwahudumia wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao ni wateja wa mkataba wa Vodacom Tanzania.Zoezi hilo limefanyika Bungeni Mjini Dodoma ikiwa sehemu ya kujali wateja wake ambapo wabunge zaidi walijiunga na huduma hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2012

    Hakuna I-pad aina ya Galaxy tablet mkuu. Ulitakiwa kusema, TABLET aina ya Samsung Galaxy.

    Chiggs

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2012

    Brother Michu hakuna iPad ya Samsung Galaxy, hizo ni bidhaa mbili tofauti.... iPad ni bidhaa ya Apple na Galaxy ni Bidhaa ya Samsung. Tafadhali rekebisha kaka.

    Mdau kutoka kilwa masoko, kwa Bibi Manyau

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2012

    Jamani..... msipotoshe.....!!! Huwezi kuwa na I-pad aina ya Samsung Galaxy....... I-pad is a trade mark... Samsung Galaxy ni trade mark... They are known as "tablets"... jamani lugha ! Jamani lugha....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2012

    Hii kali, ipad aina ya Samsung Galaxy!.....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 20, 2012

    Nimeona kitu kimoja ambacho naona mara nyingi sana katika blog mbali mbali (na hii ikiwemo) matumizi yasiyo sahihi ya lugha. Maelezo katika mojawapo ya picha yanasema ... akipokea i-Pad aina ya Samsung...
    i-Pad ni "brand name" ya tablet computer inayotengenezwa na Apple. Hivyo sio sahihi kuiita tablet computer ya samsung kama i-Pad.

    ReplyDelete
  6. Kimweri MagangaJuly 20, 2012

    Michuzi,
    iPad aina ya Samsung??? Kwi kwi kwi; kali sana hii, sijawahi kusikia kuna iPad aina ya samsung. iPad ni bidhaa ya apple, naona lugha hapa gongana kabisa. Hizi ni tablet computers, sema naona jina la iPad limetawala sana ila hii ni brand name, wasichanganye hao. Nadhani wanauza bidhaa bila ya kuwa na maelezo sahihi ya nini wanachokiuza. Ndo tunajifunza mumo humo lakini.

    Na we mzee wa libeneke nunua iPad ya Nokia basi. Kwe kwe

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2012

    Power of a brand...iPad =TABLETS, Kazi ya Steve Jobs RIP ni nzuri.jamaa was a genius.chairmannwb@gmail.com.HUREEE TO APPLE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...