Watu 17 wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570 AAM kupata ajali na kupinduka.
Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.
inasikitisha na inatia huruma , pamoja na janga hili, naomba sisi abiria ,tutumie akili zetu wenyewe kwa kujali maisha yetu ,kuliko kujali kuwahi kufika. Zebedayo msema kweli
ReplyDeletetunangoja kuja kupewa pole na sie.
ReplyDeleteDuh Poleni sana Wadau.
ReplyDeleteNauliza tue kaswali kamoja. Hii basi inauwezo wakubeba abiria wangapi!!?