Purukushani na vurugu vimeumuka leo katika mji wa Kigamboni eneo la Kisota baada ya   wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kokoto kuzuiliwa na Serikali kuendelea na shughuli hiyo.


Wananchi waliokuwa na ghadhabu walifunga barabra kwa mawe na kuwasha matairi barabarani kama inavyoonekana pichani. Inaripotiwa askari wa kuzuia fujo, FFU, walikuwa katika eneo husika ili kutuliza ghasia na kurejesha usalama wa raia na mali zao.
Picture
(picha via ukurasa wa facebook wa Dkt. Mkunde Mlay)
Picture
Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia (FFU), wakiwa wameweka doria katika barabara kuu ya kutoka Kigamboni kwenda Mji Mwema Dar es Salaam leo, baada ya kudhibiti vurugu za wachimba kokoto wa eneo la Maweni ambao walifunga barabara hiyo kwa mawe kwa zaidi ya masaa natatu na kuchoma matairi wakishinikiza kuruhusiwa kuchimba kokoto. (picha: RICHARD MWAIKENDA)
Picture
Baadhi ya mawe yaliyoondolewa barabarani baada ya kuwekwa na wachimba kokoto eneo la Maweni, Kigamboni. Watu kadhaa wanaotuhumiwa kufanya vurugu hizo wametiwa mbaroni. 

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inahabarisha kuwa vurugu kubwa limezuka muda huu huko Kigamboni maeneo ya Mji Mwema kutokana na kile kinachodaiwa kuzuiliwa kwa baadhi ya wakazi wa huko kuchimba kokoto katika sehemu ambayo imekatazwa na Serikali.

Askari wa Jeshi la polisi wamefika katika eneo hilo kuhakikisha hali inarejea kuwa shwari,lakini wananchi hao hawataki kutii amri hiyo na kuendelea kuwarushia mawe Askari hao na kufunga barabara kwa kupanga mawe makubwa,hali ambayo imehatarisha usalama wa watu wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MICHUZI HABARI ZA ASUBUHI !
    Inaonesha sio mfuatiliaji mzuri wa vipindi vya Bunge linaloendelea sasa ; nasema haya kwa sababu Mh. waziri wa Mambo ya Ndani alisema bayana kuwa wasiitwe tena "wananchi wenye ghadhabu au hasira kali" !!, bali waitwe WANANCHI WANAO JICHUKULI SHERIA MIKONONI.

    ReplyDelete
  2. Haya na hao semeni UAMSHO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...