Kushoto ni Katibu wa CCM DMV Jacob Kinyemi akiongea jambo na kumkaribisha mwenyekiti wa CCM DMV Loveness Mamuya ili awasalimie Watanzania waliojumuika pamoja kwenye Futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV siku ya Ijumaa Aug 3, 2012 Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland. Futari hiyo ilianza kwa swala ya magharibi.
Watanzania wa DMV na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV Hillandale Park.
Watanzania wakipata picha ya pamoja walipojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyofanyikia Hillandale Park Silver Spring, Maryland.
Watanzania na marafiki zao wakiwa wamechukua chakula huku wakibadilishana mawili matatu katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV.
Nguo za rangi ya kijani na njano ndizo nyingi zilizokua zimetawala ndani ya ukumbi wa Hillandale Park katika futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV.
Watanzania waliojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV wakiwa kwenye mstari wa kuchukua chakula.
Watanzania na marafiki zao wakiwa kwenye futari ya pamoja.
Watanzania waliojumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na CCM DMV wakipakua chakula
Wakina mama na watoto wao wakiwa kwenye mjumuiko huo wa futari ya pamoja.
Sheh Omar akiwa nae kwenye Futari hiyo.


Naona Sheikh Omar sahani yake si haba! hahahahahahahahahaha...
ReplyDeletewacha wee, nakuona karim banji umetakata kweli si mchezo kumbe upo majuu? nakumbuka tu mapishi yako unavyojua kukarangiza hilo halina ubishi. nakutakia mfungo mwema.
ReplyDeleteNilidhani futari ni kwa ajili ya waliofunga. Kumbe siku hizi hata wasiofunga wanafuturu.
ReplyDeleteUmma wa kiisalam naona mnajisahau sana na hivyo vyama vyenu mnaviingiza sana kwenye dinin mambo ya futari kuna haja gani kuvaa mavazi ya chama
ReplyDeleteKwenye kula hakuna chama,naamini CHADEMA wamo.
ReplyDeletemmmmhh !! hawa wote ni wazanzibari. Sasa hao jamaa wawili wanaokataa muungano na kutupigia kelele,utafikiri wako 100, tuwaiteje hao ???? mbona wanakera sana hao ??? watu tumetulia na roho zetu na tunamshukuru Mungu kwa amani aliyoipa nchi yetu, kasoro tu hawa jamaa wawili ambao nina uhakika ni Wayemenari,si warudi kwao ?? aahh!! Zebedayo msema kweli
ReplyDeletefutari na baadhi ya hayo mavazi ya kina mama hayaendani,ni kuitukana swaum na futari yenyewe.marafiki jamani huwa wanaalikwa siku ya eid kula pamoja na nk,si ktk kuftari maana hawajafunga!!!kuftari maana yake ni kufungua(kula)baada ya jua kuzama
ReplyDeletewewe zebedayo domo kaya wewe kila mahali unajifanya kusema sema utumbu, kwa taarifa yako njoo katika futari ya wazanzibar utaona mambo si hii ya ccm kwani dini ina ccm. na kwa taarifa yako uzi ule ule, tunataka nchi yetu MUUNGANO kani yao wenyewe,angalia MAlawi wanadai ziwa Nyasa itakuwa siku tunataka nchi yetu muungano basi na hatutasita mpaka kitaeleweka.
ReplyDeletesasa wewe ni mungu umeshajuwa wangapi hapo hawajafunga na wewe unajibebea dhambi za bure unahukumu sasa unajuwaje kama walifunga kuwasindikiza wenzao ?watanzania tunapata mda wa kukosoa sio wamaendeleo duu
ReplyDeleteMashalaah mwenyekiti kazi unaiweza mungu akujalie na akuepushe na husda akuepushe na majungu inshallah kheri wana dmv
ReplyDeleteUnaona ? ukweli daima unauma, na wewe kwa vile tulishakujua kwamba siyo mwenzetu,basi . Wewe endelea tu na kelele zako za utengano. wewe ni mchafuzi ,haja yako ,utuchafulie kisha ukimbilie Yemen,sasa sijui kilichokuondoa huko Yemen ni nini !!! Futari umeliona lakini na hizo t-shirts,kwa taarifa yako ,zinapicha ya nyundo na jembe na maana ya nyundo ni kanyaga twende., hakikisha passport yako inakaa mfuko wa shati Pemba to Sanaa anytime. Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteMdau Anonymous wa Sat Aug 04, 08:59:00 PM 2012
ReplyDeleteMalawi kudai ziwa Nyasa wamejidhalilisha sana na kuonekana kuwa kama wamesoma kumbe vilaza!
HIYO HATA WAKIENDA UN (UMOJA WA MATAIFA) HAWAPATI NG'O!
KWA KUWA SHERIA ZA KIMATAIFA ZINASEMA (UNESCO WORLD HERITAGE) MAZIWA NA BAHARI NI RASILIMALI ZA WOTE WANAOPAKANA NAZO HIVYO MIPAKA YAKE IMO NDANI YA MAJI KWA KUGAWANA SAWA KWA SAWA, YAANI PALE ZIWA NYASA HATA MSUMBIJI WANA ENEO LAO LA ZIWA INGAWA NI KILOMETA CHACHE SIO KIGEZO NA WAO LAZIMA WAWE NA SEHEMU YAO HIVYO KJANUNI HII YA UN-UNESCO INAWALINDA.
NDIO MAANA UNAWEZA KUONEKANA KAMA UMESOMA LAKINI UKAWA HUJAELIMIKA NDIO HAO MALAWI SASA NA MADAI YAO YA KIPUUZI.
TATIZO HUYU MAMA JOYCE BANDA RAISI WAO MPYA AMEINGIA KWA JAZBA SANA KWENYE UTAWALA NA MBAYA ZAIDI ANAFANYA MAMBO KAMA VILE HAJASOMA!.
TANZANIA INALIJUA HILI NDIO MAANA INAFAHAMU MALAWI WAMESHA CHEMKA HAWAWEZI KUSHINDA HATA WAENDE MAHAKAMA GANI DUNIANI.
Nafikiri Saver niwakati wakumshughulikia zebedayo nahisi sasa analeta chuki kila sehemu!kwakweli huyu jamaa anachefua!
ReplyDeleteKwa nini Wanawake wamevaa mavazi ya chama? Je, wao kudhani kuwa kufunga au hawawezi kuvaa chochote wanachotaka? Hii ni mbaya sana. Kuchukua rushwa kutoka CCM ni haramu. Hii ilikuwa kampeni ya kisiasa na matangazo mengi. Wakati mwingine kusubiri hadi baada ya Ramadhani kufanya shughuli zako za kawaida DMV.
ReplyDeleteSisi wanatakiwa kufunga. Kitu pekee missing hapa ni muziki.
ReplyDeleteMdau wa Sat Aug 04, 08:59:00 PM 2012
ReplyDeleteMadai ya MAlawi.......kutaka Ziwa Nyasa.
Ama kweli hapa ndipo utatambua ya kuwa kujua Kiingereza sio kuelimika!
Hawa Wamalawi wanajifanya Waingereza sana, yaani hata Lugha yao ya Kichewa karibia kila neno ni la (KichewaNGEREZA) yaani Kiingezera lakini pamoja na hilo wameshindwa kuzitambua Sheria za Kimataifa za Mipaka ambazo zimeandikwa kwa Kiingereza wanachokijua wao!
Angalieni, sijui huyo Balozi wao Malawi huko UN anafanya kazi gani?, yaani ameshindwa kumshauri vuzuri Raisi wake anamwacha akiaibika bure Duniani!