Kushoto ni Katibu wa CCM DMV Jacob Kinyemi akiongea jambo na kumkaribisha mwenyekiti wa CCM DMV Loveness Mamuya ili awasalimie Watanzania waliojumuika pamoja kwenye Futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV siku ya Ijumaa Aug 3, 2012 Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland. Futari hiyo ilianza kwa swala ya magharibi.
Watanzania wa DMV na marafiki zao wakijumuika pamoja kwenye futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV Hillandale Park.
Watanzania wakipata picha ya pamoja walipojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyofanyikia Hillandale Park Silver Spring, Maryland.
Watanzania na marafiki zao wakiwa wamechukua chakula huku wakibadilishana mawili matatu katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV.
Nguo za rangi ya kijani na njano ndizo nyingi zilizokua zimetawala ndani ya ukumbi wa Hillandale Park katika futari ya pamoja iliyotayarishwa na CCM DMV.
Watanzania waliojumuika pamoja katika futari ya pamoja iliyoandaliwa na CCM DMV wakiwa kwenye mstari wa kuchukua chakula.
Watanzania na marafiki zao wakiwa kwenye futari ya pamoja.
Watanzania waliojumuika pamoja katika Futari iliyoandaliwa na CCM DMV wakipakua chakula
Wakina mama na watoto wao wakiwa kwenye mjumuiko huo wa futari ya pamoja.
Sheh Omar akiwa nae kwenye Futari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Naona Sheikh Omar sahani yake si haba! hahahahahahahahahaha...

    ReplyDelete
  2. wacha wee, nakuona karim banji umetakata kweli si mchezo kumbe upo majuu? nakumbuka tu mapishi yako unavyojua kukarangiza hilo halina ubishi. nakutakia mfungo mwema.

    ReplyDelete
  3. Nilidhani futari ni kwa ajili ya waliofunga. Kumbe siku hizi hata wasiofunga wanafuturu.

    ReplyDelete
  4. Umma wa kiisalam naona mnajisahau sana na hivyo vyama vyenu mnaviingiza sana kwenye dinin mambo ya futari kuna haja gani kuvaa mavazi ya chama

    ReplyDelete
  5. Kwenye kula hakuna chama,naamini CHADEMA wamo.

    ReplyDelete
  6. mmmmhh !! hawa wote ni wazanzibari. Sasa hao jamaa wawili wanaokataa muungano na kutupigia kelele,utafikiri wako 100, tuwaiteje hao ???? mbona wanakera sana hao ??? watu tumetulia na roho zetu na tunamshukuru Mungu kwa amani aliyoipa nchi yetu, kasoro tu hawa jamaa wawili ambao nina uhakika ni Wayemenari,si warudi kwao ?? aahh!! Zebedayo msema kweli

    ReplyDelete
  7. futari na baadhi ya hayo mavazi ya kina mama hayaendani,ni kuitukana swaum na futari yenyewe.marafiki jamani huwa wanaalikwa siku ya eid kula pamoja na nk,si ktk kuftari maana hawajafunga!!!kuftari maana yake ni kufungua(kula)baada ya jua kuzama

    ReplyDelete
  8. wewe zebedayo domo kaya wewe kila mahali unajifanya kusema sema utumbu, kwa taarifa yako njoo katika futari ya wazanzibar utaona mambo si hii ya ccm kwani dini ina ccm. na kwa taarifa yako uzi ule ule, tunataka nchi yetu MUUNGANO kani yao wenyewe,angalia MAlawi wanadai ziwa Nyasa itakuwa siku tunataka nchi yetu muungano basi na hatutasita mpaka kitaeleweka.

    ReplyDelete
  9. sasa wewe ni mungu umeshajuwa wangapi hapo hawajafunga na wewe unajibebea dhambi za bure unahukumu sasa unajuwaje kama walifunga kuwasindikiza wenzao ?watanzania tunapata mda wa kukosoa sio wamaendeleo duu

    ReplyDelete
  10. Mashalaah mwenyekiti kazi unaiweza mungu akujalie na akuepushe na husda akuepushe na majungu inshallah kheri wana dmv

    ReplyDelete
  11. Unaona ? ukweli daima unauma, na wewe kwa vile tulishakujua kwamba siyo mwenzetu,basi . Wewe endelea tu na kelele zako za utengano. wewe ni mchafuzi ,haja yako ,utuchafulie kisha ukimbilie Yemen,sasa sijui kilichokuondoa huko Yemen ni nini !!! Futari umeliona lakini na hizo t-shirts,kwa taarifa yako ,zinapicha ya nyundo na jembe na maana ya nyundo ni kanyaga twende., hakikisha passport yako inakaa mfuko wa shati Pemba to Sanaa anytime. Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  12. Mdau Anonymous wa Sat Aug 04, 08:59:00 PM 2012

    Malawi kudai ziwa Nyasa wamejidhalilisha sana na kuonekana kuwa kama wamesoma kumbe vilaza!

    HIYO HATA WAKIENDA UN (UMOJA WA MATAIFA) HAWAPATI NG'O!

    KWA KUWA SHERIA ZA KIMATAIFA ZINASEMA (UNESCO WORLD HERITAGE) MAZIWA NA BAHARI NI RASILIMALI ZA WOTE WANAOPAKANA NAZO HIVYO MIPAKA YAKE IMO NDANI YA MAJI KWA KUGAWANA SAWA KWA SAWA, YAANI PALE ZIWA NYASA HATA MSUMBIJI WANA ENEO LAO LA ZIWA INGAWA NI KILOMETA CHACHE SIO KIGEZO NA WAO LAZIMA WAWE NA SEHEMU YAO HIVYO KJANUNI HII YA UN-UNESCO INAWALINDA.

    NDIO MAANA UNAWEZA KUONEKANA KAMA UMESOMA LAKINI UKAWA HUJAELIMIKA NDIO HAO MALAWI SASA NA MADAI YAO YA KIPUUZI.

    TATIZO HUYU MAMA JOYCE BANDA RAISI WAO MPYA AMEINGIA KWA JAZBA SANA KWENYE UTAWALA NA MBAYA ZAIDI ANAFANYA MAMBO KAMA VILE HAJASOMA!.

    TANZANIA INALIJUA HILI NDIO MAANA INAFAHAMU MALAWI WAMESHA CHEMKA HAWAWEZI KUSHINDA HATA WAENDE MAHAKAMA GANI DUNIANI.

    ReplyDelete
  13. Nafikiri Saver niwakati wakumshughulikia zebedayo nahisi sasa analeta chuki kila sehemu!kwakweli huyu jamaa anachefua!

    ReplyDelete
  14. Kwa nini Wanawake wamevaa mavazi ya chama? Je, wao kudhani kuwa kufunga au hawawezi kuvaa chochote wanachotaka? Hii ni mbaya sana. Kuchukua rushwa kutoka CCM ni haramu. Hii ilikuwa kampeni ya kisiasa na matangazo mengi. Wakati mwingine kusubiri hadi baada ya Ramadhani kufanya shughuli zako za kawaida DMV.

    ReplyDelete
  15. Sisi wanatakiwa kufunga. Kitu pekee missing hapa ni muziki.

    ReplyDelete
  16. Mdau wa Sat Aug 04, 08:59:00 PM 2012

    Madai ya MAlawi.......kutaka Ziwa Nyasa.

    Ama kweli hapa ndipo utatambua ya kuwa kujua Kiingereza sio kuelimika!

    Hawa Wamalawi wanajifanya Waingereza sana, yaani hata Lugha yao ya Kichewa karibia kila neno ni la (KichewaNGEREZA) yaani Kiingezera lakini pamoja na hilo wameshindwa kuzitambua Sheria za Kimataifa za Mipaka ambazo zimeandikwa kwa Kiingereza wanachokijua wao!

    Angalieni, sijui huyo Balozi wao Malawi huko UN anafanya kazi gani?, yaani ameshindwa kumshauri vuzuri Raisi wake anamwacha akiaibika bure Duniani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...