| MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI PICHA NA .www.burudan.blogsports.com |
| MTUHUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA |
| MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO. Picha zaidi BOFYA HAPA |


Hili limekuwa tatizo kubwa sana kwetu Tanzania ...miaka mingi. Hata vikao vya haki miliki vya kimataifa vimetutaja... Enzi zake marehemu Remmy Ongala alikua akilia sana lakini ilikuwa kama kusukuma ukuta. Mbali na muziki kuna pia suala la baadhi ya wanahabari/ mabloga kutumia kazi za wenzao (mathalan picha) bila kusema au kukiri wamezitoa au kuzichopoa wapi. Safi Ankal umelimeweka hadharani maana hili ni suala la ajira kwa wafanyakazi wa sanaa...popote walipo.
ReplyDeletejamani hata mlie machozi ya damu bado kazi zenu hazita achwa kuibiwa kwanza hapo ndo kwanza mnawapa sababu wagonga copy kuendeleza wizi... kwani hamuoni movie zenu zikiwa uploaded kwenye mtandao?? nakumbuka nilipo kua bongo hata kwenye cable wanaonyesha alafu nasikia mnalipwa laki 2 hahahaha jamni hii ni raha tena san
ReplyDeleteTanzania tunaongoza kwa watu kupenda fedha rahisi rahisi na za bure.!!!
ReplyDeleteUnakuta mtu huyo anayefanya biashara ya wizi wa kurudufu kazi za Wasanii anaishi kwa kujigamba,dharau,sifa na jeuri kumbe anaishi kwa wizi mtupu!
Hongereni sana kina JB na Mtunis pamoja na wasanii wengine. Hii kazi ilikuwa ifanywe na COSOTA, sijui wamelala wapi?
ReplyDeleteInatia sana uchungu hao wasanii wanavyohangaika bila msaada wowote, then unakuta wajanja wachache wako kivulini wanafaidi jasho la watoto wa wenzao. Kwenye picha ya pili anaonekana mtuhumiwa, ambaye ni kabwana mdogo tu jamani.
Hivi mnajua ni vifaa gani vinavyotumika kufanya kazi ya kihuni kama hii? Hadi alama za siri na nembo za wasanii zimechakachuliwa??? Please people. Huyo bwana mdogo akipelekwa pale Central Police, akaingizwa kule basement kwenye vyumba vya interrogation, atawataja wahusika wakuu walio nyuma yake.
Na mtashangaa jinsi watu walivyo washenzi! Kuna wenzetu hawa wenye ajili ya kinanii, ambao kwanza ni wazuri sana kwa masuala ya IT, wanavyo vifaa vya kucheza na graphics za aina yoyote na mitambo kibao ya kuchakachua hata sura za watu ili mradi wapate picha za wahusika.
Ifike mahali Serikali iwe serious ili Sanaa iweze kinufaisha vijana wa nchi hii kama ilivyo kwa wenzetu wa Nigeria, Ghana, n.k.
Wasanii, mkiona vipi itabidi mwende wenyewe huko Nigeria na Ghana mkajifunze wao walitatua vipi Changamoto ya uchakachuaji kama huu wa kazi za sanaa. Sidhani kama nchi yetu ina wajanja zaidi ya Nigeria. All the best wasanii wa TZ. Msikate tamaa, mtafika tu!