Mkurugenzi wa kitengo cha kodi ya mapato za kimataifa nchini Viet Nam Bw Nguyen Duc Thinh, Afisa elimu Mwandamizi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DSM Bibi Lucina Shayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo kikuu cha Kodi ya Mapato Nchini Viet Nam, Ofisa wa Kodi za Kimataifa katika serikali ya Viet Nam bi Dinh Thi Bich Hao na Mtaalam wa Kodi za Kimataifa wa serikali ya Viet Nam Bw Cung Quang Hung.
Bibi Lucina Shayo akitoa maelezo ndani ya ukumbi wenye michoro ya Mapangoni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo kikuu cha Kodi ya Mapato Nchini Viet Nam, Bi Le Hong Hai akipiga ngoma ya Kinyawezi iliyotumika kuhamasisha ufanyaji kazi, huku kushoto Mkurugenzi wa kitengo cha kodi ya mapato za kimataifa nchini Viet Nam Bw Nguyen Duc Thinh akiigiza kama analima kwa kufuata mdundo wa ngoma hiyo.
Mkurugenzi wa kitengo cha kodi ya mapato za kimataifa nchini Viet Nam Bw Nguyen Duc Thinh akimwonyesha Bi Lucina Shayo umahiri wa matumizi ya Ungo uliopo katika ukumbi wa Mila na Desturi uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo kikuu cha Kodi ya Mapato Nchini Viet Nam, Bi Le Hong na Mkurugenzi wa kitengo cha kodi ya mapato za kimataifa nchini Viet Nam Bw Nguyen Duc Thinh kwamasikitiko wakiziangalia sanamu zinazoonesha namana Biashara ya Utumwa ilivyofanyika hapa nchini.

Na Mdau Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa.

Viongozi wakuu waandamizi na maafisa wa kodi katika serikali ya Viet
Nam wameitembelea Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kujionea kujifunza mambo mbali yanayohusu Tanzania kwa kupitia vioneshwa vilivyomo katika kumbi mbali mbali za Makumbusho hiyo.

Akielezea madhumuni ya ziara yao makumbusho hapo, Mkurugenzi wa kitengo cha kodi ya mapato za kimataifa nchini Viet Nam Bw Nguyen Duc Thinh alisema ni kujifunza mambo muhimu yanayo dhaminiwa na watanzania, na kufahamu utajiri mkubwa wa historia ya nchi hii, ameeleza kuwa wamefurahia sana kuona baadhi ya mambo ya Utamaduni wa watanzania unafanana na ule wa nchini kwao hasa katika matumizi ya vifaa mbali mbali vya kutendea kazi.

Uongozi huo umeupongeza Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kwa mapokezi mazuri na huduma nzuri uliyowapatia katika ziara waliyoifanya makumbusho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huu ungo ndio makumbusho yaliyobaki, inatia imani mshauza kila kitu umangani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...